Wezi wavamia makazi ya Kocha Carlo Ancelotti wapora sanduku la fedha

Jeshi la Polisi mjini Merseyside limesema kuwa, watu wawili ambao walikuwa wamevalia mavazi ya kujihami kwa slaha pamoja na kujifunika uso kwa kwa vifunika uso vyeusi wamevamia makazi ya Meneja na Kocha wa Everton, Carlo Ancelotti yaliyopo Crosby nchini Uingereza, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Inadaiwa baada ya wahalifu hao kuyavamia makazi hayo usiku wa kuamkia jana Jumamosi walimkuta binti yake huku wakichukua sanduku lenye fedha na kutokomea nalo kusikojulikana.

Polisi wamesema, wahalifu baada ya kumkuta binti wa kocha huyo mwenyewe nyumbani, waliamua kuondoka na sanduku hilo ambalo bado haijafahamika kulikuwa na kiasi gani cha fedha.

Kocha Ancelotti ambaye ni raia wa Italia aliteuliwa kuiongoza Everton mwezi Desemba, 2019 ambapo alisaini mkataba wa miaka minne na nusu katika dimba la Goodison Park nchini humo.

No comments

Powered by Blogger.