KIKOSI CHA WACHEZAJI 24 WA KMC KUWAFUATA POLISI TANZANIA JIJINI ARUSHA KESHO

Kikosi cha KMC FC kesho kitaondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Jijini Arusha katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Machi Nne katika uwanja wa Sheikhe Amri Abeid.
Katika msafara huo wa wana Kino Boys, utakuwa na wachezaji 24, Benchi la ufundi pamoja na Viongozi ambapo KMC FC inakwenda Jijini Arusha kusaka alama tatu muhimu ikiwa ugenini.

Aidha KMC FC katika mchezo huo inakwenda ikiwa imejipanga kupata ushindi ambapo katika michezo ya nyumbani imefanya vizuri kwa michezo miwili mfululizo ya Ligi kuu sambamba na mchezo mmoja wa michuano ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa magoli matano kwa mawili dhidi ya Kurugenzi kutoka Mkoani Simiyu.

Kino Boys inahitaji ushindi katika mchezo huo kwani katika duru ya kwanza ilipoteza mchezo dhidi ya wapinzani wake Polisi Tanzania kwa kuifunga goli moja kwa sifuri katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Kesho tunakwenda kuwafuata Polisi Tanzania, tunasafiri tukijua kuwa tunakwenda kucheza na timu ambayo ni nzuri, lakini KMC FC tunahitaji ushindi katika mchezo huo licha ya kwa mba tutakuwa ugenini, lakini tuna kumbukumbu nzuri katika mchezo uliopita.

Hata hivyo KMC FC inasaka ushindi katika michezo miwili Ugenini ambapo mbali na Polisi Tanzania, itakutana na Coast Union ya Jijini Tanga Jumapili Machi saba katika uwanja wa Mkwawani.

Imetolewa na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya KMC

Post a Comment

0 Comments