Rais Dkt.Mwinyi amteua mrithi wa Maalim Seif nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Zanzibar).

Katika taarifa ya vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said ilieleza kwamba kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 9(3)cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kinachosema kwamba “Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa wa Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia”.

Hivyo, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 39(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, baada ya kushauriana na Chama cha ACT-Wazalendo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemtea Othman Masoud Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 01 Machi, 2021. Sherehe ya kuapishwa kwa Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar itafanyika kesho tarehe 02 Machi, 2021 saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Ikulu, Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news