Rais Samia aongoza marais, viongozi, Watanzania kuaga mwili wa Hayati Dkt.Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 22 Machi, 2021 amewaongoza Watanzania, Wakuu wa Nchi na Serikali, wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na viongozi mbalimbali kutoa heshima za mwisho Kitaifa kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, anaripoti Mwandishi Maalum DIRAMAKINI (Dodoma).
Akizungumza katika tukio hilo, Mhe. Rais Samia amewashukuru Waheshimiwa Marais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na wawakilishi wa Wakuu wa Nchi waliokuja kuungana na Watanzania katika kutoa heshima za mwisho kwa Hayati Dkt. Magufuli na ameeleza kuwa ujio wao na jinsi Watanzania walivyoonesha mapenzi yao tangu msiba huu mkubwa wa Kitaifa utokee vimedhihirisha kuwa Dkt. John Pombe Magufuli alikuwa kipenzi cha watu.

Mhe. Rais Samia amesema Hayati Dkt. Magufuli alikuwa mwalimu, kiongozi na mlezi wake na kwamba alihusudu utendaji wake kwa namna alivyokuwa mfuatiliaji na msimamizi wa miradi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akilihutubia Taifa na Viongozi wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa mbalimbali Duniani kwenye Mazishi ya Kitaifa ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri JIjini Dodoma leo March 22,2021.
Gari Maalumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ likiwa limebeba Jeneza lenye Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati likiwasili katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kwa ajili ya shughuli ya kuagwa Kitaifa leo tarehe 22 Machi 2021.

Makamanda wa JWTZ wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati wakiwasili katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Makamanda wa JWTZ wakipiga Saluti mara baada ya kuweka Jeneza lenye Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika chumba maalumu kwa ajili ya shughuli ya kuagwa na viongozi mbalimbali. Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Felix Tshisekedi akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Amebainisha kuwa Taifa limepoteza kiongozi mahiri, shupavu, jasiri, mchapakazi, muadilifu, mnyenyekevu, mcha Mungu, mfuatiliaji, mzalendo kwa Taifa lake, mtetezi wa wanyonge, mwanamwema wa Afrika, mwanamageuzi mahiri, mwanamapinduzi wa kweli, mtu asiyekuwa na makuu na mtumishi wa wote.

Mhe. Rais Samia ameeleza kuwa wakati wa uongozi wake, Hayati Dkt. Magufuli aligusa maisha ya watu wengi na kwa muda mfupi, na kwamba kwa kipindi alicholiongoza Taifa alijikita kujenga uchumi wa ndani unaotegemea mapato ya ndani, kusimamia rasilimali za Taifa ili zifaidishe wananchi kwa kuziba mianya ya rushwa na upotevu wa mapato, kufufua na kuwekeza katika miradi ya kimkakati kama vile kufufua Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) kwa kununua ndege na ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere, ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge railway – SGR) ili kufanikisha azma ya ujenzi wa viwanda ambavyo vinahitaji miundombinu wezeshi. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma

Rais wa Zambia Edgar Lungu akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitoa Heshima za Mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Amesema katika kipindi chake cha uongozi, Tanzania ilipata Makamu wa Rais mwanamke ambaye leo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amewahakikishia Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuwa yeye na viongozi wenzake wapo tayari kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na kwamba yale aliyoyakusudia yatafikiwa.

Mhe. Rais Samia amewaondoa shaka walio na wasiwasi juu ya hatma ya Tanzania baada ya Hayati Dkt. Magufuli kufariki dunia kuwa kila kitu kitakuwa sawa “Kwa wale ambao wana mashaka mwanamke huyu ataweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nataka niwaambie aliyesimama hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
Mama Janeth Magufuli Mjane wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli akilia kwa uchungu wakati akitoa Heshima za mwisho kwenye Jeneza la mme wake katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. (Picha zote na Ikulu).

Amewataka Watanzania kumuenzi Hayati Dkt. Magufuli kwa kutekeleza yote mazuri aliyoyafanya katika ujenzi wa Taifa.

Ameihakikishia familia ya Hayati Dkt. Magufuli kuwa Taifa linatambua mchango mkubwa ambao ameutoa na kwamba atakuwa nao na kuwashika mkono siku zote.

Mhe. Rais Samia amewahakikishia nchi marafiki na majirani wa Tanzania kuwa Tanzania itaendelea kuwa jirani mwema na mshirika mzuri katika ushirikiano wa kikanda na kimataifa, na kwamba uhusiano wake utaimarika zaidi katika kipindi chake cha uongozi.

Katika salamu zao, Marais 9 wa nchi mbalimbali za Afrika wamemshukuru Hayati Dkt. Magufuli kwa utumishi wake wakati wa uhai wake ambapo alionesha mfano wa namna Afrika inavyoweza kujiamulia mambo yake yenyewe, kujitegemea, kujenga uchumi wake, kupiga vita rushwa na kuwapigania watu wake.

Wamempongeza Mhe. Rais Samia kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wamemhakikishia ushirikiano na uhusiano mzuri katika kipindi chote cha uongozi wake.

Dkt. John Pombe Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Machi, 2021 Jijini Dar es Salaam kwa maradhi ya moyo na atazikwa tarehe 26 Machi, 2021 nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.

Post a Comment

0 Comments