Serikali ya Tanzania yatoa maelekezo kwa mabalozi wake kote Duniani

Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nje ya Nchi wameelekezwa kujipanga, kushiriki na kutafuta fursa zitakazowezesha bidhaa mbalimbali za Tanzania kupata masoko ya uhakika katika nchi walizopo, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akisisitiza jambo kwenye Kikao kazi na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kilichofanyika jijini Dodoma.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akizungumza na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na kuongeza kuwa , Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatamka bayana juu ya diplomasia ya uchumi sambamba na kuimarisha sauti ya Tanzania na taswira yake katika medani ya uhusiano wa kikanda na kimataifa.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa ili kufanikisha hilo Balozi zinapaswa kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika jumuiya nyingine za kimataifa zikiwemo, Indian Ocean Rim Association, Indian Ocean Tuna Commission, South South Commission, South West Indian Ocean Fisheries Commission.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Tate Olenasha (Mb) akizungumza na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoiwakilisha nchi sehemu mbalimbali Duniani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kwenye kikoa kazi kilichofanyika jijini Dodoma.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert A. Ibuge akisisitiza jambo katika Kikao kazi katika ya Mhe. Prof Kabudi na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Mabalozi na Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) kwenye Kikao Kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

Aidha amewataka Mabalozi hao kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoyatoa wakati akizundua Baraza la Wawakilishi ya kutaka Uchumi wa Bluu kupitia uvuvi wa Bahari Kuu unakuwa na manufaa kwa Wananchi hususani katika kuongeza mapato, ajira na kukuza uchumi kwa kuzingatia kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni ya Muungano.

Pia Prof. Kabudi amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) katika maendeleo ya Taifa na kuzielekeza Balozi zianze na ziboreshe kanzi data ya Diapora ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kuanzisha Jumuiya zao.
Sehemu nyingine ya Mabalozi na Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) kwenye Kikao Kazi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani mara baada ya Kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo baada ya Kikao Kazi kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu mbalimbali Duniani mara baada ya kuhitimisha Kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

“Natambua kazi hiyo inaendelea na kwa sasa tuna data za diaspora takriban 98,658 na kuna jumuiya 77 za diaspora. Nichukue fursa kusisitiza umuhimu wa Balozi zetu kuboresha na kuharakisha zoezi hili kwa kubuni njia mbalimbali za kuwaandikisha,"amesema Prof. Kabudi.

Mkutano huo wa Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi umehudhuriwa pia na Naibu Waziri, Mhe William Tate Ole Nasha, Katibu Mkuu Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news