Tangazo lililodai Rais Samia amefariki Daily News lawang'oa wafanyakazi ofisini

Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) imewaachisha kazi Anitha K. Shayo ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Matangazo na Rajab Juma Mohammed ambaye ni Msimamizi wa Dawati la Huduma kwa Wateja, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Wawili hao wameachishwa kazi ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za kushindwa kuzuia makosa kwenye tangazo la pongezi walilotoa katika Gazeti la Daily News la Machi 29, 2021
Kipande cha sehemu ya tangazo hilo kilichosambaa mtandaoni kiliandikwa ‘Congratulation, The board of Director, Management and Staff of STAMICO join fellow Tanzanians in mourning the death of H.E President Samia Suluhu Hassan for being sworn in as the 6th president of United Republic of Tanzania’

Katika hatua nyingine TSN wamesitisha huduma za mwakilishi wa kujitegemea wa matangazo, Lameck Samson

Post a Comment

0 Comments