Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today March 31st, 2021

UTABIRI WA SIKU TANO ZIJAZO UMETOLEWA LEO TAREHE 31/03/2021
..........................

JUMATANO: Tarehe 31-03-2021

1. ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Katavi, Kigoma, Tabora, Rukwa, Songwe na Mbeya.


UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI

2. ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

Athari zinazoweza kujitokeza;

Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi na usafirishaji.

Tafadhali zingatia na ujiandae.

............................
ALHAMISI 01-04-2021

1. ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Tanga, Pwani (inayojumuisha visiwa vya Mafia) na Dar es salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

2. ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.)

UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

Athari zinazoweza kujitokeza;

Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi usafirishaji.

Tafadhali zingatia na ujiandae.

...............................

IJUMAA 02-04-2021

HAKUNA TAHADHARI

................................

JUMAMOSI 03-04-2021

HAKUNA TAHADHARI.

...............................


JUMAPILI 04-04-2021

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es salaam, Tanga,, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Mtwara, Lindi, pamoja na visiwa vya Unguja and Pemba.

UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI

KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

Athari zinazoweza kujitokeza;

Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji.

Tafadhali zingatia na ujiandae.

............................


Utabiri huu umetolewa

Na, MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Post a Comment

0 Comments