Wasifu wa Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli

Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959 huko Chato Mkoani Geita. Alipata Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Chato kuanzia 1967 hadi 1974. 

Mwaka 1975 alijiunga na Seminary ya Katoke na kisha Sekondari ya Lake Mwanza hadi 1978 alipohitimu
Mwaka 1979 alijiunga na Sekondari ya Upili ya Mkwawa, Iringa kwa masomo ya Kidato cha Tano na Sita na kuhitimu 1981. Mwaka 1981 hadi 1982 alisomea Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa Sayansi katika Chuo cha Ualimu cha Mkwawa, Iringa.

Alijiunga na Chuo cha UDSM mwaka 1985 hadi 1988 alipotunukiwa Shahada ya Ualimu katika masomo ya Kemia na Hisabati. Mwaka 1991 hadi 1994 alisomea Shahada ya Uzamili ya Kemia UDSM na Chuo Kikuu cha Salford, Uingereza.

Mwaka 2009 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alifanya kazi kama Mkemia katika Chama cha Ushirika cha Nyanza huko Mwanza hadi mwaka 1995.

Oktoba 2015 alitangazwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa JMT na mnamo Oktoba 2020 alitangazwa tena kuwa Rais kwa Muhula wa Pili ambapo amehudumu kwa takriban miezi 4 mpaka umauti ulipomkuta.

Hayati John Magufuli alifunga ndoa na Janeth mwaka 1989 na ameacha Watoto saba ambao ni Suzana, Edna, Mbalu, Joseph, Jesca, Yuden na Jeremia, pamoja na wajukuu kumi.


Credit:JamiiForums.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news