Waziri Mkuu Majaliwa aeleza kifo cha Hayati Dkt.Magufuli kinavyompa shida

Kila ninapoona jeneza la Rais John Magufuli, siamini macho yangu, nahisi kama vile napigiwa simu napewa maagizo na maelekezo, imekuwa siku ngumu sana kwangu. Sina kubwa la kusema, waliotagulia wamesema mengi kuhusu mpendwa wetu. Binafsi napata shida kusema, naona kama vile ananipigia simu, ananipa maagizo, naomba mnivumilie, ni siku ngumu kwetu.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati Wabunge walipouaga mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Machi 22, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Kassim Majaliwa ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema, kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinampa shida kwani kila wakati akikaa anahisi kama anamuongelesha kwa kumpa maagizo kwa ajili ya kuyatekeleza, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dodoma).

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo Machi 22, 2021 wakati akizungumza Bungeni jijini Dodoma ambapo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipata nafasi ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kila wakati anahisi kama anaongea na Hayati Magufuli hivyo inampa shida na wakati mgumu.

"Sijui niseme nini huu msiba ni mzito mno, yaani mpaka sasa inanipa shida,nikikaa nahisi kama naongea nae, ananipa maagizo au wakati mwingine nahisi kama ananipigia simu, kwa kweli Dkt. Magufuli ametuachia fumbo,"amesema.

Amesema, anamshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Dkt. Magufuli kwani ameacha alama katika nchi hii na amewatendea mema Watanzania kwa kuwajali kwa vitendo.

"Hayati Dkt.Magufuli ameacha alama katika majimbo yetu,kila mwenye macho ameona,ushahidi umeonekana kwa jinsi wananchi walivyomlilia Dar es Salaamskwa siku mbili,lakini hata Dodoma watu walipanga foleni barabarani mpaka usiku mwili ulipokuwa ukipita,"amesema Majaliwa.

Post a Comment

0 Comments