MUHIMBILI WAJIBU KWA HOJA PENDEKEZO LA MHESHIMIWA DKT.HAMISI KIGWANGALLA LA KUTAKA MASHINE ZA KUJIFUKIZA KUONDOLEWA MUHIMBILI

Kuna ujumbe wa sauti ya Mbunge wa Nzega Mjini, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambao pamoja na mambo mengine anataka huduma ya kujifukiza iliyoanzishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuvunjwa kwa kuwa inaleta picha mbaya.
Mbunge wa Nzega Mjini, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla. (Picha na Maktaba).

Uongozi wa Hospitali unapenda kutoa ufafanuzi kuwa;

Ugonjwa wa Covid 19 ni ugonjwa mpya ambao hadi sasa duniani hakuna mwenye majibu sahihi.

Majibu sahihi yanatokana na tafiti zinazofanywa sehemu mbalimbali duniani kwa sasa. Tafiti hizi zinaanza na wazo ambalo wataalamu wanalifanyia kazi kisayansi na kutoa majibu. Kwa muda kumekuwa na taarifa kuwa tiba asilia ikiwemo kujifukiza kunasaidia katika tiba ya Covid 19.

Aidha, tafiti mbalimbali kutoka sehemu nyingine duniani kama Israel na Italia zimeongelea kujifukiza (steam therapy) kama njia mojawapo ya tiba ya ugonjwa huu na mengine ya upumuaji.

Kwa mantiki hii MNH iliona kuna umuhimu wa kuleta huduma hii ili wananchi walio tayari waitumie na pia wataalamu wapate nafasi ya kuifanyia utafiti kwa njia za kisayansi na kutoa majibu sahihi kama inafaa au haifai.

Hii pia itatoa nafasi kwa wataalamu wetu kuwa sehemu ya mjadala wa tiba ya Covid 19 unaoendelea kote duniani badala ya kuwa pembeni na kusubiri kila wazo au jibu kutoka kwa wenzetu. 

Na hii pia inawakumbusha wataaalamu wetu kwamba tunachokikubali kuwa ni njia sahihi kimeanza kwa namna hii na watalaamu wetu wawe tayari kufanya utafiti na kuchangia kutoa majibu yanayohitajika badala ya kusibiri kila kitu tufanyiwe na kuletewa mezani.

Aidha mpaka sasa zaidi ya wananchi 1,100 wakiwemo wataalamu wa afya (madaktari, wauguzi n.k) waliotumia huduma hii wametoa taarifa ya kuridhishwa na huduma hii.

Sasa ni muhimu wataalamu wetu wa design study ambayo itatupa majibu sahihi.

Aidha Hospitali ya Taifa Muhimbili yenye dhamana ya kutoa elimu, kutibu na kufanya utafiti itakua inatimiza malengo na majukumu yake.

Kwa muktadha huu MNH, haitaondoa huduma hiyo kwa kuwa iko kwenye utekelezaji sahihi wa majukumu yake ya kitafiti kama wanavyofanya wanasayansi wengine kote duniani.

Imetolewa na;

Aminiel Aligaesha

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano

Hospitali ya Taifa Muhimbili

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news