Rais Dkt.Mwinyi atoa tamko kampuni inayodaiwa kutapeli wananchi Bilioni 38.5/

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itafanya kila juhudi kuhakikisha inapata fedha zilizopo mikononi mwa Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd ili hatimae zirudi mikononi mwa wananchi waliowekeza, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, akitowa taarifa ya Serikali kuhusiana na Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd, iliyokuwa ikiendesha shughuli za kifedha ikiwemo kupokea amana na kutoa mikopo kinyume cha Sheria na taratibu za Nchi, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar Aprili 6, 2021.(Picha na Ikulu).

Dkt.Mwinyi amesema hayo Ikulu jijini Zanzibar alipokuwa akitoa taarifa ya Serikali, kuhusiana na shughuli zilizokuwa zikifanywa na Kampuni ya Masterlife Microfance Ltd hapa Zanzibar, kwa waandishi wa habari.

Amesema, Kampuni ya Masterlife Microfanance Ltd iliosajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Tanzania Bara pamoja na Bodi ya Mapato Tanzania (TRA), haikutekeleza majukumu yake ya kufuga wanyama na kusindika vyakula kwa mujibu wa usajili na badala yake iliendesha shughuli za kukusanya fedha kwa wananchi.
Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani ) akitowa taarifa ya Serikali kuhusiana na Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd, ilikuwa ikiendesha shughuli za kifedha kinyume na sheria, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Mwandishi wa habari wa gazeti la Dailynews Zanzibar Ndg. Masato Masato akiuliza swali kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kutoa taarifa ya Serikali kuhusiana na Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Zanzibar leo Bi. Mwantanga Ame akiuliza swali wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akitowa taarifa wa Serikali kuhusiana na Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd, iliyokuwa ikitowa huduma za Kifedha, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Mwandishi wa habari wa ITV Ndg. Farouk Karim akiuliza maswali wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akitowa taarifa ya Serikali kwa Waandishi wa habari kuhusiana na Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd, ilioko Zanzibar, mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Amesema, uchunguzi uliofanywa na taasisi zinazohusiana na uendeshaji wa biashara za kifedha, umebaini kamapuni hiyo haikuwa na biashara inayotoa faida na badala yake ilikuwa ikizungusha fedha hizo miongoni mwa wateja wake.

Amesema, kutokana na utaratibu huo idadi ya wanachama iliongezeka kutokana na shauku ya kupata faida kubwa waliyopewa watu waliowekeza mwanzoni, hatua inayofanya kiwango cha fedha kinachohitaji kulipwa kuwa kikubwa kuliko makusanyo.

Amesema, kampuni hiyo imeleta mtafaruku mkubwa kwa wananchi, ikizingatiwa kiwango kikubwa cha fedha za Kitanzania zipatazo Bilioni 38. 5 kilichowekwa na wananchi wanaokadiriwa kufikia 39,000.

“Hali hii imeleta taharuki katika nchi yetu kwa vile wananchi walikuwa na matumaini makubwa na biashara hiyo, kwani baadhi walijiunga kwa kuchukua mikopo mikubwa kutoka benki ziliopo nchini,”amesema.

Aidha, amesema biashara hiyo haikuwa halali kwa vile fedha zilizowekezwa hazionekani katika benki zilizopo nchini.

Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali inaendelea na uchunguzi wa shauri hilo na pale utakapokamilika italifikisha suala hilo kwenye vyombo vya sheria kwa uamuzi.

Amesema, tayari Serikali imezuia jumla ya shilingi Bilioni 4.79 kutoka maeneo mbalimbali yaliowekezwa na mmiliki wa Kampuni hiyo pamoja na mali mbalimbali, ikiwemo magari ya kifahari, bidhaa na majengo anazomiliki.

Amewataka wananchi kuwa waangalifu na kuepuka kujiingiza katika biashara za aina hiyo, sambamba na kuwataka kuwa wastahamilivu pamoja na kutoa mashirikiano kwa vyombo vya dola kadri itakavyohitajika.

Amesema, Serikali inaendelea na uchunguzi na ufuatiliaji wa kampuni na taasisi zinazojishughulisha na biashara zisizofuata taratibu na kusababisha madhara ya kiuchumi kwa Serikali na wananchi wake.

Aidha,amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha haki za wananchi waliowekeza kwa mujibu wa sheria zinalindwa kadri itakavyowezekana kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Mnamo Machi 4, 2021 Serikali ilichukuwa hatua ya kuizuia Kampuni ya Masterlife Microfanance Ltd kuendelea na shughuli zilizokuwa zikiendeshwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa kufanya shughuli hizo kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news