Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today April 1st, 2021

 UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 01/04/2021

.............................
Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
.............................
Mikoa ya Mwanza, Kagera, Geita, Mara, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Tabora na Katavi: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
...............................
Mikoa ya Mbeya, Njombe, Songwe, Iringa, Rukwa, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Ruvuma na Morogoro: inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua
................................
Mikoa ya Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
...............................
ANGALIZO
VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA MAENEO MACHACHE YA MIKOA YA DAR ES SALAAM, TANGA NA PWANI (IKIJUMUISHA VISIWA VYA MAFIA) LINDI , MTWARA, PAMOJA NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA
................................
KIWANGO CHA JUU CHA JOTO NI NYUZI JOTO 32 ( 32°C ) KATIKA MJI WA TANGA NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA.
................................
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kutoka Kusini kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa.
Matarajio kwa siku ya Jumamosi tarehe 03/04/2021: Mabadiliko kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 01/04/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Post a Comment

0 Comments