BIASHARA UNITED MARA WAICHAPA NAMUNGO FC 2-0

TIMU ya Biashara United Mara imetinga hatua ya Nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) baada ya kuichapa Timu ya Namungo FC kutoka mkoani Lindi mabao 2-0 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Mjini Musoma, ANARIPOTI AMOS LUFUNGULO (Diramakini).
Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi na kusisimua, timu ya Biashara United Mara ilipata bao la kwanza dakika ya 8 lililowekwa kimiani na mchezi wake Mpapi Nasibu.

Mchezo uliendelea kwa kasi huku Biashara United Mara wakipambana kuongeza bao jingine na Namingo FC wakitaka kusawazisha.

Biashara United Mara waliweza kupata bao la pili lililofungwa na Kelvin Friday dakika ya 38 kwa mkwaju wa penati baada ya mcheziji wa Biashara United Mara, Tarick Simba kuchezewa madhambi eneo la hatari.

Hadi mchezo huo ulikwenda mapumziko timu ya Biashara United Mara wakiwa mbele kwa mabao 2, huku timu ya Namungo FC wakiwa 0.

Kipindi Cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikicheza kwa bidii na kufanya mabadiliko kuhakikisha kwamba inapata matokeo. Lakini safu za ulinzi za timu zote mbili zilikuwa imara kuzuia mashambulizi.

Hadi mchezo huo unamalizika Timu ya Biashara United Mara imeibuka na ushindi wa mabao 2-0

Mwenyekiti wa Timu ya Biashara United Mara Seleman Mataso akizungumza na Waandishi wa Habari amepongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kujituma kwa bidii na kuzingatia maelekezo ya Mwalimu. Huku akiwapongeza Waamuzi wa mchezo huo kwa kuchezesha mpira huo kwa haki

Post a Comment

0 Comments