🔴𝐋𝐈𝐕𝐄: Rais Samia mgeni rasmi sherehe za Mei Mosi 2021 kitaifa jijini Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Mei Mosi,2021 ndiye mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka huu ambapo kitaifa yanafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, anaripoti MWANDISHI DIRAMAKINI.
Awali Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU, Gerson Msigwa amesema, Rais atalihutubia taifa, atapokea maandamano, risala ya wafanyakazi, atatoa zawadi kwa wafanyakazi bora na atatoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya Mei Mosi.

Aidha, hii ni mara ya kwanza kwa Rais Samia kuhudhuria kama mgeni rasmi katika sherehe hizi toka aape kuwa Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Post a Comment

0 Comments