Rais Samia, Museveni washuhudia utiaji saini mkataba hodhi kati ya Tanzania na EACOP

Na Diramakini (diramakini@gmail.com)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni leo tarehe 20 Mei, 2021 wameshuhudia utiaji saini wa mkataba hodhi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki litakalojengwa kuanzia Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Mei, 2021.

Hafla ya utiaji saini mkataba huo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Mawaziri, viongozi wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Wabunge, Makatibu Wakuu, wawakilishi kutoka kampuni za uwekezaji wa CNOCC ya China na Total ya Ufaransa na wawakilishi kutoka Sekta binafsi.

Kwa upande wa Tanzania mkataba huo umetiwa saini na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Matogolo Kalemani na kushuhudiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi wakati upande wa kampuni ya EACOP umetiwa saini na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Martin John Tiffen na kushuhudiwa na Rais wa Utafiti na Uzalishaji wa Total Afrika Bw. Nicolas Terraz.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wa nyimbo za Mataifa mawili ya Tanzania na Uganda zikipigwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Waziri Kalemani amesema utiaji saini wa mkataba huu umekamilisha hatua zote za majadiliano na sasa kinachoendelea ni kuanza kwa kazi za ujenzi wa bomba litakalokuwa na urefu wa kilometa 1,443 ambapo kati yake kilometa 1,147 zitajengwa katika ardhi ya Tanzania.

Ujenzi wa mradi huu unaotarajiwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 4.16 utakamilika katika kipindi cha miaka 3 ambapo utakuwa na uwezo wa kusafirisha mapipa 216,000 ya mafuta ghafi kwa siku, utahusisha ujenzi wa vituo 8, ujenzi wa vituo vya kulainisha mabomba ya chuma 29, ujenzi wa valvu 76 na ujenzi wa matanki 5 yenye uwezo wa kuhifadhi mapipa laki 5 ya mafuta kila moja katika Bandari ya Tanga.

Tanzania na Uganda kila moja inamiliki asilimia 15 ya hisa zote za kampuni hiyo, na kutokana na umiliki huo Tanzania itapata asilimia 60 ya mapato na Uganda itapata asilimia 40 na kutokana na mapato ya Dola za Marekani Milioni 290 zinazotarajiwa katika kipindi cha miaka 25 ya uhai wa mradi, Tanzania itapata mapato ya Dola za Marekani Milioni 59, itapata kodi ya kiasi cha Dola za Marekani Milioni 73, fedha za kigeni zitaongezeka kwa asilimia 53 na ajira zaidi ya 10,000 katika Mikoa 8, Wilaya 24, Kata 134, Vijiji 257 na Vitongoji 527 ambako bomba litapita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Nchi hodhi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania)katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Nchi hodhi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania)katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini mkataba wa Tamko la Pamoja kati ya Tanzania na Uganda kuhusu utekelezaji wa pamoja Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania)katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini mkataba wa Tamko la Pamoja kati ya Tanzania na Uganda kuhusu utekelezaji wa pamoja Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania)katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake, Mhe. Rais Samia amemshukuru aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyeanza mchakato wa mradi huu pamoja na Mhe. Rais Museveni, amewapongeza Mawaziri, Makatibu Wakuu na kamati za majadiliano za Tanzania na Uganda kwa kufanikisha kuanza kwa mradi huo.

Ameahidi kuwa Tanzania itauendeleza, kuuenzi, kuukuza na kuuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kirafiki, kidugu na kihistoria kati yake na Uganda ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mradi huu unafanikiwa kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na Uganda.

Mhe. Rais Samia amesema anaamini kuwa mradi huo utachochea juhudi za pamoja za utafutaji mafuta na gesi katika nchi za ukanda huu zikiwemo Tanzania, DRC, Burundi na Sudan Kusini na pia utawavutia wawekezaji wengi zaidi kuja kuwekeza Tanzania na nchi nyingine za ukanda huu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini mkataba wa Tamko la Pamoja kati ya Tanzania na Uganda kuhusu utekelezaji wa pamoja Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania)katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akitia saini mkataba wa Tamko la Pamoja kati ya Tanzania na Uganda kuhusu utekelezaji wa pamoja Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania)katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wamkisikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula wakati akisoma maazimio ya Tamko la Pamoja kuhusu utekelezaji wa pamoja wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania)katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakiwa wameshika nyaraka za Tamko la pamoja kuhusu utekelezaji wa pamoja wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania)katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wanahabari waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa nchi hodhi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki la kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania)
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wanahabari waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa nchi hodhi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki la kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wanahabari waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa nchi hodhi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki la kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wanahabari waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa nchi hodhi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki la kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania).Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wanahabari waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa Mkataba wa nchi hodhi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki la kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania).
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipiga makofi pamoja na viongozi wengine wa ndani na nje ya Nchi mara baada ya hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango mara baada ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa nchi hodhi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki la kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi Wakuu wa Vyombo ya Ulinzi na Usalama mara baada ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa nchi hodhi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki la kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleane Tanga (Tanzania). (PICHA ZOTE NA IKULU).

Kwa upende wake, Mhe. Rais Museveni amesema moja ya changamoto kubwa alizoziona katika safari yake ya kupigania ukombozi na maendeleo ya Afrika ni kukosekana kwa mwelekeo lakini kuanza kwa mradi huu ni uthibitisho kuwa sasa mwelekeo unaonekana.

Amefafanua kuwa katika kutafuta ustawi wa jamii, pamoja na kusimamia sekta za huduma za jamii zinazojumuisha elimu, afya, maji na usalama ni lazima kusimamia uzalishaji mali utakaosaidia kupata utajiri na fedha kama vile kilimo, viwanda, huduma na tehama ambazo kwa pamoja zinahitaji uwepo wa miundombinu bora na nishati.

Hata hivyo, Mhe. Rais Museveni ameonya kuwa mradi wa bomba la mafuta usisababishe Tanzania na Uganda kubweteka na kuacha kusimamia ipasavyo sekta za kudumu za uzalishaji mali kwa kuwa mafuta yana mwisho.

Mhe. Rais Samia na Mhe. Rais Museveni wametia saini tamko la pamoja la utekelezaji wa mradi huo (Communiqué) na kisha Mhe. Rais Museveni amerejea nchini Uganda.

Post a Comment

0 Comments