SHILATU ASISITIZA USAJILI REJESTA ZA MAKAZI

Afisa Tarafa ya Mihambwe wilayani Newala Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Ulinzi na Usalama Tarafa ya Mihambwe, Emmanuel J. Shilatu amesisitiza Wenyeviti wa vitongoji, Wenyeviti wa vijiji washirikiane na Watendaji vijiji na Watendaji kata kuhakikisha wanasajili wakazi wa kudumu na wageni kwenye rejesta ya makazi kwenye maeneo yao.
Hayo yamebainishwa kwenye kikao kazi ambapo aliwaeleza viongozi hao kufanya hivyo ili kuweka taarifa sahihi za Wakazi wa kudumu na kubaini taarifa sahihi za wageni.

“Tuendelee kuweka mkazo kwenye usajili rejesta za makazi kwa wakazi wa kudumu na kubaini wageni wote na kutambua taarifa zao. Kazi hii iendelee kwa ushirikiano kuanzia ngazi za vitongoji, vijiji na kata wote tutimize wajibu wetu ipasavyo. Mlinzi wa amani na usalama ni Mimi, wewe na yule, ni sisi sote,”amesisitiza Gavana Shilatu.
Wakati huo huo, Gavana Shilatu alifanya ziara kutembelea ofisi za vijiji na kata kukagua rejesta za makazi ambapo alisisitiza maboresho ya mara kwa mara ya taarifa ziendane na wakati na hali ilivyo kwa sasa.

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Tarafa.

Post a Comment

0 Comments