WANAWAKE WA NCAA WAFANYA UTALII WA NDANI KWA KUTEMBELEA VIVUTIO VILIVYOPO MKOANI TANGA

Na Kassim Nyaki-NCAA (Tanga)

Watumishi wanawake kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) mwishoni mwa wiki wamefanya ziara ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko mkoani Tanga kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhamaisha utalii wa Ndani.
Watumishi wa NCAA wakiwa katika mapango ya Amboni mkoani Tanga ikiwa ni ziara maalum ya kutembelea vivutio vya vya mkoa huo kama sehemu ya kuhamasisha Utalii wa Ndani.Ujumbe wa wanawake hao unaojumuisha Maafisa na Askari wa NCAA umetembelea vivutio vilivyoko Mapango ya amboni yanayosimamiwa na kuendelezwa na NCAA pamoja na kutembelea msitu wa Hifadhi ya Magoroto uliopo Muheza Mkoani Tanga.

Kaimu Kamishna msaidizi Mwandamizi anayesimamia Uhusiano wa Umma Joyce Mgaya amebainisha kuwa ziara hiyo imelenga kuwajengea uwezo wanawake hao kujifunza kwa vitendo shughuli mbalimbali za uhifadhi katika maeneo mengine ya Nchi yaliyohifadhiwa vizuri kwa kuyatembelea na kuona yanavyotunzwa pamoja na kujenga mahusiano na taasisi nyingine zinazojishughulisha na masuala ya Uhifadhi.

“Katika Hifadhi ya Ngorongoro tuna majukumu ya Uhifadhi, Utalii na maendeleo ya Jamii, kama wadau wa utalii tumeona tutumie fursa ya mwisho wa wiki kutembelea vivutio tofauti na kujifunza zaidi shughuli za kiuhifadhi zinazofanywa na wenzetu katika mazingira asilia kama haya yam situ wa Magoroto na mapango ya amboni yenye historia nzuri na ya kuvutia” aliongeza Joyce Mgaya.
Watumishi wanawake wa NCAA wakiwa katika picha ya pamoja katika msitu wa Hifadhi ya Magoroto Wilayani Muheza Mkoani Tanga.

Afisa Uhifadhi mkuu wa NCAA Bi. Flora Assey akiwa katika ziara hiyo ameeleza kuwa fursa hiyo wameitumia vizuri kujifunza masuala mbalimbali ya uhifadhi kuona namna jitihada za watu binafsi wanavyoweza kutumza msitu wa wa Magoroto wenye kilimota za mraba zaidi ya 1000 ambao umeongeza fursa za utalii na kuwa chanzo cha maji kwa zaidi ya asilimia 75 ya wakazi wa wilaya ya Muheza.

Wakiwa katika ziara ya kutembelea mapango ya Amboni Mkoani Tanga watumishi hao wameeleza kufurahishwa na uwepo wa eneo mapango ya amboni ambayo yana vivutio vingi na vya kipekee vinavyomfanya mtalii atamani kurudi zaidi ya mara moja kutokana na upekee wa eneo hilo.
Watumishi wanawake wa NCAA wakiwa katika mlango mkuu wa kuingia mapango ya Amboni mkoani Tanga kwa ajili ya kutembelea vivutio vilivyopo katika eneo hilo.

Mkuu wa Hifadhi ya Mapango ya amboni Bw. Melckzedek Mwambugu amewashukuru watumishi hao kutenga muda wa kutembelea vivutio hivyo na kutoa wito kwa Wanzania wengie kutembelea vivutio vilivyopo katika mapango ya amboni ambayo kwa sasa miundombinu ya Utalii imezidi kuboreshwa ikiwemo uwekaji wa taa maalum, ujenzi wa daraja ndani na pango linalosaidia watalii kutembea kwenye mazingira bora zaidi.

Post a Comment

0 Comments