REA yawatunuku Tuzo Mhandisi Zena na Mheshimiwa Mgalu

Na Veronica Simba -REA

Bodi ya Nishati Vijijini (Rural Energy Board – REB) imetunuku Tuzo za utumishi uliotukuka katika kusimamia usambazaji wa umeme vijijini kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said na aliyekuwa Naibu Waziri Subira Mgalu.
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhandisi Zena Said (wa pili-kulia) na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu (wa pili-kushoto) wakionesha Tuzo walizotunukiwa na Bodi ya Nishati Vijijini (REB), katika Hafla maalumu, Juni 28, 2021 jijini Dodoma, kutokana na utendaji wao mahiri katika sekta ya nishati vijijini, walipotumikia Wizara ya Nishati kwa Nafasi ya Katibu Mkuu na Naibu Waziri (mtawalia). Kushoto ni Mjumbe wa Bodi Oswald Urassa aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga.

Viongozi hao walitunukiwa Tuzo hizo Juni 28, 2021 jijini Dodoma, katika Hafla iliyoandaliwa na Bodi hiyo kwa kushirikiana na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyolenga kuwashukuru kwa mchango wao walioutoa katika sekta husika.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi husika, Oswald Urassa, aliwapongeza viongozi hao akisema utendaji wao katika sekta ya nishati umeacha alama chanya isiyoweza kufutika kutokana na kuwa na maslahi mapana kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Oswald Urassa akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo, katika Hafla maalumu ya kuwapongeza na kuwatunuku Tuzo Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhandisi Zena Said pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu (hawapo pichani) kutokana na utendaji wao mahiri katika sekta ya nishati vijijini, walipotumikia Wizara ya Nishati kwa Nafasi ya Katibu Mkuu na Naibu Waziri (mtawalia). Hafla hiyo ilifanyika Juni 28, 2021 jijini Dodoma.

Akifafanua, Urassa alisema Bodi na Wakala kwa ujumla wanaamini kuwa utendaji mahiri wa Mhandisi Zena katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, ndiyo uliomwezesha kuaminiwa na kuteuliwa kushika wadhifa alionao sasa wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu akizungumza katika Hafla maalumu ya kumpongeza na kumtunuku Tuzo yeye pamoja na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhandisi Zena Said (kushoto), kutokana na utendaji wao mahiri katika sekta ya nishati vijijini, walipotumikia Wizara ya Nishati kwa Nafasi ya Naibu Waziri na Katibu Mkuu (mtawalia). Hafla hiyo iliandaliwa na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) na ilifanyika Juni 28, 2021 jijini Dodoma.

Kwa upande wa Subira Mgalu, Urassa alieleza kuwa REA inajivunia utendaji na uongozi wake uliokuwa shirikishi na uliolenga kuhakikisha kazi ya kusambaza umeme vijijini inatekelezwa kwa ufanisi, kasi, ari na weledi.

“Kutokana na utendaji wenu mahiri, Bodi imeona ni vyema tutambue mchango wenu uliotuwezesha kufika hapa tulipo leo ambapo vijiji zaidi ya 10,000 vya Tanzania Bara vimefikiwa na umeme kati ya 12,268 vilivyopo,” alisema.
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhandisi Zena Said, akizungumza katika Hafla maalumu ya kumpongeza na kumtunuku Tuzo yeye pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu (hayupo pichani) kutokana na utendaji wao mahiri katika sekta ya nishati vijijini, walipotumikia Wizara ya Nishati kwa Nafasi ya Katibu Mkuu na Naibu Waziri (mtawalia). Hafla hiyo iliandaliwa na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) na ilifanyika Juni 28, 2021 jijini Dodoma.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena alitoa shukrani kwa Wizara ya Nishati, REA na taasisi zote zilizo chini ya Wizara hiyo kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote alichotumikia kwa nafasi ya Katibu Mkuu.

“Kupitia ninyi nyote, niliweza kuonekana na kuaminika hata nikateuliwa kuwatumikia wananchi wa Zanzibar kupitia nafasi hii ya Katibu Mkuu Kiongozi. Nawashukuru sana,” alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga akizungumza katika Hafla maalumu ya kuwapongeza na kuwatunuku Tuzo Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhandisi Zena Said pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu (hawapo pichani) kutokana na utendaji wao mahiri katika sekta ya nishati vijijini, walipotumikia Wizara ya Nishati kwa Nafasi ya Katibu Mkuu na Naibu Waziri (mtawalia). Hafla hiyo iliandaliwa na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) na ilifanyika Juni 28, 2021 jijini Dodoma.

Katika hatua nyingine, alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kupitia Shirika lake la Umeme (ZECO) inalo la kujifunza kutoka REA, hususani katika mbinu za usambazaji umeme vijijini kwa kasi.
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhandisi Zena Said (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu (kushoto) wakipongezana baada ya kutunukiwa Tuzo na Bodi ya Nishati Vijijini (REB), kutokana na utendaji wao mahiri katika sekta ya nishati vijijini, walipotumikia Wizara ya Nishati kwa Nafasi ya Katibu Mkuu na Naibu Waziri (mtawalia). Hafla hiyo ilifanyika Juni 28, 2021 jijini Dodoma.

“Kwa mipango iliyopo katika Serikali yetu, ya Uchumi wa Bluu, tunahitaji umeme zaidi. Hivyo, wataalam wetu wanaweza kuona nini wachote kutoka huku kwa ajili ya kusaidia kupeleka umeme vijijini kwa kasi zaidi.”

Naye Mheshimiwa Mgalu, aliipongeza Bodi husika inayoongozwa na Wakili Julius Kalolo huku akiielezea kuwa ni ya mfano wa kuigwa kutokana na utendaji kazi wa kiubunifu na wenye viwango unaohusisha pamoja na mambo mengine kutembelea maeneo mbalimbali inakotekelezwa miradi ya umeme vijijini, ili kujionea maendeleo yake na kutoa maelekezo pale inapobidi.

“Mmenipa ari ya kuendelea kuishauri Serikali na kuisimamia katika kutekeleza kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo. Nitaendelea kushirikiana na ninyi kwa maslahi mapana ya Taifa,” alisisitiza Mgalu.

Viongozi hao walishukuru kwa Tuzo walizotunukiwa huku wakieleza kuwa zitabaki kuwa kumbukumbu ya kudumu katika vizazi vyao.
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhandisi Zena Said (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu (kushoto) wakikata keki katika Hafla maalumu iliyoandaliwa na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) kuwapongeza na kuwatunuku Tuzo kutokana na utendaji wao mahiri katika sekta ya nishati vijijini, walipotumikia Wizara ya Nishati kwa Nafasi ya Katibu Mkuu na Naibu Waziri (mtawalia). Hafla hiyo ilifanyika Juni 28, 2021 jijini Dodoma.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Dailin Mghweno akizungumza katika Hafla maalumu ya kuwapongeza na kuwatunuku Tuzo Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhandisi Zena Said pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu (hawapo pichani) kutokana na utendaji wao mahiri katika sekta ya nishati vijijini, walipotumikia Wizara ya Nishati kwa Nafasi ya Katibu Mkuu na Naibu Waziri (mtawalia). Hafla hiyo ilifanyika Juni 28, 2021 jijini Dodoma.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Loius Accaro akizungumza katika Hafla maalumu ya kuwapongeza na kuwatunuku Tuzo Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhandisi Zena Said pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu (hawapo pichani) kutokana na utendaji wao mahiri katika sekta ya nishati vijijini, walipotumikia Wizara ya Nishati kwa Nafasi ya Katibu Mkuu na Naibu Waziri (mtawalia). Hafla hiyo ilifanyika Juni 28, 2021 jijini Dodoma.
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhandisi Zena Said (wa tatu-kushoto walioketi) na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu (wa tatu-kulia walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamoja na Menejimenti na baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) baada ya Hafla maalumu ya kuwapongeza na kuwatunuku Tuzo kutokana na utendaji wao mahiri katika sekta ya nishati vijijini, walipotumikia Wizara ya Nishati kwa Nafasi ya Katibu Mkuu na Naibu Waziri (mtawalia). Hafla hiyo ilifanyika Juni 28, 2021 jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments