Watakiwa kutunza nidhamu wawapo lindoni

Na Doreen Aloyce, Diramaki Blog

KAMISHNA Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Chacha Jackson amewataka wahitimu wa mafunzo ya ulinzi wa kampuni ya ulinzi ya Shima Gaurd ambayo ipo chini ya Jeshi la Magereza kudumisha nidhamu kazini kwa kujiepusha kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa uvunjaji benki na tamaa ambazo zinaweza kuwaangamiza.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye kufunga mafunzo ya wahitimu 104 yaliyofanyika kwa mwezi mmoja na kufanikiwa kwa weledi mkubwa.

Kamishna Chacha ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magereza amesema kuwa, kuna baadhi ya walinzi ambao wamekuwa wakichafua taasisi kutokana na ukosefu wa maadili kwa kujihusisha na wizi wawapo makazini kwa kuvunja mabenki kuiba fedha jambo ambalo ni kinyume na sheria za ulinzi.

"Mmepewa mafunzo ya mwezi mmoja na kufundishwa mbinu zote za kijeshi na nimeona umahiri wenu kutoka kwa walimu sasa niwaombe mkawe kioo katika jamii , mkawahudumie wateja kama mlivyoelekezwa na sio kuwaudhi, nitashangaa kama mtakuwa miongoni mwa wahalifu wanaojihusisha na ujambazi na tamaa.

"Nidhamu ni kitu muhimu sana sio kumsalimia mtu shikamoo!la hasha ni kuhakikisha mnakuwa wakakamavu kuanzia kuamka mapema,kuvaa vizuri sio mlegezo muonekano wa mavazi mpaka utendaji kazi lazima muwe na nidhamu kwenye biashara zenu,"amesema.

Amesema kuwa, shirika hilo linamilikiwa na Serikali na wamepewa kibali cha kufanya biashara kwa kuanzisha kampuni tanzu ikiwa ni pamoja na hili shirika la ulinzi kinachotakiwa ni wajitume kwani shirika lina mpango wa kuanzisha kampuni nyingi za usafi na uwakala wa bima hivyo nidhamu ya biashara ni muhimu jambo litakalosaidia kuheshimika na kupata kazi nyingi.

Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kenneth Mwambije amesema kuwa, walichojifunza kilete matokeo kwa kutambua kuwa Jeshi la Magereza linadhamiria kuja na Mapinduzi katika ulinzi kwa kuwasaidia vijana kupata ajira hivyo nidhamu yao itaifanya kampuni hiyo ya Shima Gaurd kukua.

Nae Afsa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Shima Guard, Msemwa Omary alisema kampuni Tanzu ya Jeshi la Magereza ilianzishwa kwa lengo la kutoa huduma za ulinzi hapa nchini na kwamba kwa sasa ina vituo vitatu katika Mkoa wa Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam huku wakijipanga kupanua wigo katika mikoa mingine.

"Tumewapa mafunzo mengi ambayo yatawasaidia kwenye utendaji kazi wao ikiwemo nidhamu na utii,ukakamavu, kujiamini ,saikolojia ,sheria ,polisi jamii ,huduma inayojali mteja,na huduma ya kwanza,"amesema Omary.

Awali akisoma risala mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo Mohamed Jeradi amesema kuwa, katika mafunzo wamekabiliwa na changamoto muda wa kozi,uchakavu wa sare za mafunzo na ukosefu wa makazi kwa wanaotoka mbali,huku wakiiomba Jeshi kuboresha changamoto hizo kwa kuwapatia hostel na bajeti ya matibabu wakati wa majunzo yajayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news