PASS Leasing Company LTD yazinduliwa kuwapatia mikopo wakulima bila dhamana

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

Waziri wa Kilimo, Prof.Adolf Mkenda amezindua kampuni mpya ya PASS Leasing Company LTD inayomilikiwa na Taasisi ya PASS Trust yenye lengo la kutoa mikopo ya zana za kilimo bila dhamana yoyote.
Akizungumza jijini Dodoma wakati akizindua kampuni hiyo pamoja na ufungaji wa wiki ya Taasisi ya PASS Trust (Private,Agriculture Sector Support Trust) iliyoandaliwa na taasisi hiyo kuanzia Julai 21 hadi Julai 24 kwa lengo la kuchagiza masuala ya kilimo nchini.

Prof.Mkenda amesema kuwa, lengo ya wiki ya PASS ilikuwa ni kuwakutanisha wakulima,wauza zana za kilimo,taasisi za kifedha,wauza pembejeo,viongozi wa Serikali na wachakataji katika kuzungumzia masuala ya upatikanaji wa fedha kama kichocheo cha ukuaji wa kilimo biashara.

“PASS imekuwa itoa dhamana ya mikopo kuanzia asilimia 20-60 hadi asilimia 80 kwa wanawake kwa benki shiriki kama njia ya kuongeza dhamana ya kutosha ili kuwezesha wateja kupata mikopo,”amesema.

Hata hivyo ameipongeza PASS kwa kuandaa wiki hiyo kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali na kuwataka kwenda kujifunza zaidi na kuwa bora kutokana na kongamano hilo.

Aidha, amesema kuwa Serikali inatarajia kuleta mbegu bora za alizeti na kuzigawa kwa mkataba kwenye viwanda vinavyozalisha zao hilo hali itakafanya soko hilo kuwa la uhakika na kuondoa uhaba wa Mafuta unaojirudia kila Mwaka.

“Serikali itawajibika kwa kuwawezesha wakulima kwa kuwapelekea wataalamu wa zao la alizeti,na tutaweka masharti kuwa ukivuna alizeti unamuuzia mwenye kiwanda ili kuhakikisha viwanda vyote vinavyoingia mkataba vinazalisha mafuta kwa mwaka mzima,”amesema.

Pia Prof.Mkenda ametumia nafasi hiyo kuzitaka benki zote nchini kutoa fursa ya mikopo kwa wakulima na kushusha riba ili kuchochea kilimo cha zao hilo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wakulima wengi zaidi kukifanya kilimo kuwa biashara.

“Ukitaka kupambana na umaskini Tanzaniana, unaweza kufanya mambo mengi Sana lakini ukweli ni kwamba umaskini utaaisha kwa kilimo,ukitaka mali utaipata shambani,”amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo, Dkt.Tausi Akida amesema kuwa, changamoto za mitaji kwa wakulima nchini bado zipo nyingi na kwamba ipo haja kwa Taasisi za fedha kuongeza kiwango kwa wakulima.

“Ili kuweka tija kwenye mazao ya kimkakati tunapaswa kuongeza nguvu katika kukuza zao la alizeti na zabibu ili kusapoti viwanda vya uchakataji ,kwa upende wetu tumeanza na programu kwa mikoa ya Simiyu,Dodoma,Singida na Morogiro kwa Kutoa pembejeo,”ameeeleza.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema ili kufanikisha maendeleo ya kilimo mkoani hapa inatarajia kusajili kaya laki 3 zinazostahili kufanya kilimo biashara na kuwa fahari kwa jiji hili.

”Mazao ya zabibu na alizeti kuwa ya kimkakati ili Kufanikisha hilo nitatumia nafasi yangu kwa kushauriana na Wizara ya kilimo kuona namna ya kuongeza ufanisi kwa mazao hayo,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news