NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateuwa Julai 10, 2021 kushika nyadhifa tofauti katika wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Nd.Mussa Haji Ali kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Katika hafla hiyo
iliyofanyika Ikulu jijini leo Julai 12, 2021 Zanzibar na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa Serikali, Dkt. Mwinyi alimuapisha Mussa Haji Ali
kuwa Katibu Mkuu (OR), Ikulu pamoja na Issa Mahafoudh Haji kuwa Katibu
Mkuu (OR) Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.
Wengine
ni Dkt. Habiba Hassan Omar kuwa Katibu Mkuu (OR) Kazi, Uchumi na
Uwekezaji na Mikidadi Mbarouk Mzee kuwa Naibu Katibu Mkuu (OR) Tawala za
Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.
Aidha, alimuapisha Aboud Hassan Mwinyi kuwa Naibu Katibu Mkuu (OR) Fedha na Mipango anayeshughulikia Fedha na Mipango.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Nd.Issa Mahfoudh Haji kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Dk.Habiba Hassan Omar akila kiapo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Kazi,Uchumi na Uwekezaji katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dk.Habiba Hassan Omar kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Kazi,Uchumi na Uwekezaji katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Mikidadi Mbarouk Mzee akila kiapo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Nd,Mikidadi Mbarouk Mzee kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
Aboud Hassan Mwinyi akila kiapo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kuwa Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango, Anayeshuhulikia(Fedha na Mipango),katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Nd,Aboud Hassan Mwinyi kuwa Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango, Anayeshuhulikia(Fedha na Mipango),katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Miongoni
mwa waliohudhuria katika hafla hiyo ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa
Rais, Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman
Abdalla, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu na Katibu wa Baraza
la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmeid Said.
Wengine
ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Said Haji, Mufti wa
Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Kitwana
Idrisa Mustafa, mawaziri, wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja
na wanafamilia.
Tags
Habari