Waziri Bashungwa afungua ukurasa mpya kwa wadau wa habari

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ametoa mwaliko kwa kutoa mnaoni kwenye marekebisho ya kanuni za utangazaji na maudhui mtandaoni.

Hayo yameelezwa leo Agosti 19, 2021 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,John Mapepele kupitia taarifa aliyoitoa kwa umma.
"Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa,
anawakaribisha wadau wa Sekta ya Habari nchini hasa wanaojihusisha na Huduma
za Utangazaji na masuala ya utoaji maudhui kwa Umma kupitia mitandao, redio na
televisheni kutoa maoni katika Rasimu ya Marekebisho ya Kanuni za Maudhui
Mtandaoni za Mwaka 2020 pamoja na Kanuni za Maudhui ya Utangazaji katika
Redio na Televisheni za Mwaka 2018.

"Marekebisho haya yamefanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 165 cha Sheria ya Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010. Maboresho hayo yatazifanya Kanuni hizo
ziendane na maendeleo ya teknolojia pamoja na kuongeza wigo wa upatikanaji wa
habari kwa wananchi.

"Rasimu za marekebisho ya Kanuni hizo zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara
(www.habari.go.tz) pamoja na tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA
(www.tcra.go.tz). Maoni yawasilishwe kwa anuani za barua pepe zifuatazo: hglsu@habari.go.tz na
amina.nguli@habari.go.tz.

"Pia, Wizara inawakaribisha wadau wa huduma za utangazaji nchini kufika katika
mkutano wa wadau Agosti, 26, 2021, katika Ukumbi wa PSSSF (Zamani - LAPF)
Jijini Dodoma, kuanzia Saa 2.00 Asubuhi ili kuhitimisha zoezi la utoaji maoni. Wote
mnakaribishwa,"ameeleza;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news