Naibu Waziri Masanja atoa mwelekeo wa Tanzania nchini Ivory Coast katika Sekta ya Utalii Afrika

Na Happiness Shayo-WMU

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itaendelea kushirikiana na nchi za Umoja wa Afrika ili kuendeleza utalii kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi wanachama.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akicheza ngoma za asili alipowasili katika mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani jijini Abidjan nchini Ivory Coast leo Septemba 27,2021.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiwasalimia machifu wa makabila mbalimbali ya nchini Ivory Coast katika mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani jijini Abidjan nchini leo. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Mary Masanja (Mb) katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani 2021 yaliyofanyika jijini Abidjan nchini Ivory Coast leo Septemba 27,2021.

“Lengo kuu la kushiriki katika maadhimisho haya ni kujifunza na kuangalia namna ya kuendeleza utalii wetu hasa katika kipindi hiki cha kukabiliana na janga la Uviko-19 lililoikumba Dunia,”amesisitiza Mhe. Masanja.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Sofitel Hotel jijini Abidjan nchini Ivory Coast kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Utalii yanayofanyika leo. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Richie Wandwi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akifuatilia ya Siku ya Utalii Duniani Jijini Abidjan nchini Ivory Coast leo. Kulia kwake ni Waziri wa Maendeleo ya Utalii wa nchini Chad, Faycal Ramat Issa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akishiriki Jukwaa la Mawaziri wa Bara la Afrika katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani Jijini Abidjan nchini Ivory Coast leo.

Aidha, Mhe. Mary Masanja ameongeza kuwa ushiriki huo ni fursa ya kubadilishana uzoefu na pia kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania ikiwa ni moja ya juhudi za kuunga mkono kazi anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza utalii duniani.

Kauli mbiu ya Siku ya Utalii Duniani kwa mwaka huu ni “Utalii kwa Maendeleo Shirikishi/ Jumuishi”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news