Wananchi Lushoto wapokea kwa wingi chanjo ya UVIKO-19

Na Yusuph Mussa, Lushoto

WANANCHI wa Kata ya Lushoto katika Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wameonesha mwitikio mkubwa katika kuchanja chanjo ya ugonjwa wa virusi vya korona (UVIKO-19) baada ya kujitokeza kwa wingi kwenye Uzinduzi wa uchanjaji Awamu ya Pili wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Kalisti Lazaro (wa pili kushoto) akishuhudia mwananchi akichanja chanjo ya UVIKO 19 hadharani kwenye uzinduzi wa uchanjaji wa Awamu ya Pili chanjo ya UVIKO 19 Wilaya ya Lushoto uliofanyika Septemba 27, 2021 kwenye Soko Kuu mjini Lushoto. Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Shaaban Shekilindi 'Bosnia' (kushoto) na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Lucy Maliyao (wa tatu kushoto). (Picha na Yusuph Mussa).

Kwenye uzinduzi huo uliofanyika Septemba 27, 2021 katika Uwanja wa Soko Kuu la Lushoto, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Kalisti Lazaro alikuwa mgeni rasmi, jumla ya watu waliojitokeza kuchanja papo hapo ni 26, hivyo kufanya waliojitokeza kwa wilaya nzima ya Lushoto kwa siku hiyo ya uzinduzi kufikia 111.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Lucy Maliyao amesema, chanjo walizopewa zilikuwa 3,450, na idadi ya chanjo zilizochanjwa kabla ya jana ni 1,126.

Maliyao ambaye ni Muuguzi Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya hiyo amesema, tangu kuanza kwa zoezi la uchanjaji Agosti 5, 2021 hadi Septemba 27, 2021, jumla ya wananchi 1,237 wamechanja.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Kalisti Lazaro (wa tatu kushoto) akishuhudia mwananchi akichanja chanjo ya UVIKO 19 hadharani kwenye uzinduzi wa uchanjaji wa Awamu ya Pili chanjo ya UVIKO 19 Wilaya ya Lushoto uliofanyika  Septemba 27, 2021 kwenye Soko Kuu mjini Lushoto. Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Shaaban Shekilindi 'Bosnia' (wa pili kushoto), Katibu wa CCM Wilaya ya Lushoto, Ramadhan Mahanyu (kushoto) na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Lucy Maliyao (wa nne kushoto). (Picha na Yusuph Mussa).
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Kalisti Lazaro (wa pili kushoto) akishuhudia mwananchi akichanja chanjo ya UVIKO 19 hadharani kwenye Uzinduzi wa uchanjaji wa Awamu ya Pili chanjo ya UVIKO 19 Wilaya ya Lushoto uliofanyika jana Septemba 27, 2021 kwenye Soko Kuu mjini Lushoto. Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto Shaaban Shekilindi 'Bosnia' (kushoto) na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Lucy Maliyao (wa tatu kushoto). (Picha na Yusuph Mussa).

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkuu wa Wilaya aliwataka wananchi wasipuuze ugonjwa wa UVIKO 19 kwani upo na unaua, hivyo ili kujinusuru na kifo ama madhara makubwa mara mtu apatapo ugonjwa huo, hawana budi kuchanja chanjo iliyotolewa bure na Serikali.

Lazaro alisema ana uzoefu na ugonjwa huo, kwani mmoja wa vijana wake kwenye ofisi yake, aliumwa UVIKO 19, na matibabu aliyopata Hospitali ya Wilaya ya Lushoto, na baadae KCMC yaligharimu zaidi ya sh. milioni tano. Na hiyo ni kwa sababu alifikia hatua ya kuwekwa kwenye oksijeni.

"Msifanye mzaha na chanjo. Msitanie, kwani kijana wangu alikaa siku tisa kwenye oksijeni. Na ukichukulia gharama alizotumia hospitalini kuanzia Lushoto na KCMC ni zaidi ya sh. milioni tano. Jiulize wewe utaweza kulipa gharama za matibabu sh. milioni tano? chanja, kwani chanjo itakusaidia hata ukiumwa usiweze kulazwa na kuwekewa oksijeni,"amesema Lazaro.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Kalisti Lazaro (wa pili kushoto) akishuhudia mwananchi akichanja chanjo ya UVIKO 19 hadharani kwenye Uzinduzi wa uchanjaji wa Awamu ya Pili chanjo ya UVIKO 19 Wilaya ya Lushoto uliofanyika jana Septemba 27, 2021 kwenye Soko Kuu mjini Lushoto. Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto Shaaban Shekilindi 'Bosnia' (kushoto) na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Lucy Maliyao (wa tatu kushoto). (Picha na Yusuph Mussa).
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Kalisti Lazaro (wa pili kushoto) akishuhudia mwananchi akichanja chanjo ya UVIKO 19 hadharani kwenye Uzinduzi wa uchanjaji wa Awamu ya Pili chanjo ya UVIKO 19 Wilaya ya Lushoto uliofanyika jana Septemba 27, 2021 kwenye Soko Kuu mjini Lushoto. Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto Shaaban Shekilindi 'Bosnia' (kushoto) na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Lucy Maliyao (wa tatu kushoto). (Picha na Yusuph Mussa).
Wananchi wakipata chanjo kwenye gari la wahudumu wa afya lililowekwa kwenye Uzinduzi wa Uchanjaji Awamu ya Pili Wilaya ya Lushoto uliofanyika Soko Kuu mjini Lushoto jana Septemba 27, 2021. (Picha zote Yusuph Mussa).

Mbunge wa Jimbo la Lushoto Shaaban Shekilindi 'Bosnia' aliwaomba wananchi kuchanja chanjo hiyo kwani itawasaidia kuwaondoa na hatari ya kupata madhara makubwa hata kama watapata virusi vya UVIKO 19.

Katibu wa CCM Wilaya ya Lushoto Ramadhan Mahanyu alisema Rais Samia Suluhu Hassan anawajali wananchi wake ndiyo maana akaleta chanjo hiyo, kwani Tanzania sio kisiwa, na Watanzania wenyewe ni mashuhuda kuwa ugonjwa huo upo nchini. Na ili kuonesha njia, Rais Samia alikuwa wa kwanza kuchanja.

"Kumbukeni maneno ya mheshimiwa Rais wakati anazindua chanjo, alisema yeye ni mama, ana watoto, ana wajukuu. Pia yeye ni Rais na ni Amiri Jeshi Mkuu. Hivyo kwa majukumu hayo, hawezi kuhatarisha maisha yake na Watanzania. Ni kwamba chanjo hiyo ni salama,"amesema Mahanyu.

Zoezi hilo la chanjo linaendelea leo Septemba 30, 2021 kwenye Kata ya Migambo, kwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalisti Kazaro, na Mbunge wa Jimbo la Lushoto Bosnia kufanya mkutano wa hadhara, kwani pamoja na mambo mengine, wanahamasisha wananchi kuchanja chanjo ya UVIKO 19, lakini wahudumu wa afya pia watakuwepo kuendelea kuwachaanja wananchi papo hapo, huku wahudumu wa afya wakiendelea kuchanja kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Post a Comment

0 Comments