BREAKING NEWS: Tanzania kupokea ndege zake mpya aina ya Airbus A220-300

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Ndege mpya mbili aina ya Airbus A220-300, zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania zimeondoka nchini Canada kuja Tanzania.
Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ndege hizo zitapokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume Mjini Unguja, Zanzibar kesho Oktoba 8, 2021 majira ya saa 9:00 Alasiri na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Ndege hizi zitakamilisha hesabu ya ndege 11 zilizonunuliwa na kuwasili hapa nchini.

Ndege nyingine 5 (Boeing 787-8 Dreamliner (2), Airbus A220-300 (2) na Bombardier Dash 8 Q400 (1) zimeshalipiwa na zitakuja baadaye.

Post a Comment

0 Comments