PROF.MSANJILA:SEKTA YA MADINI IMEPENDELEWA KWENYE SENSA 2022

Na Tito Mselem, Morogoro

Imeelezwa kuwa, Sensa ya Watu na Makazi ambayo inatarajiwa kufanyika Mwaka 2022, itahusisha kipengele maalum kitakachokuwa na maswali yatakayokuwa yakikusanya takwimu za wachimbaji ili kujua idadi yao, mahali walipo na mchango wao kwenye pato la taifa.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (mbele kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Hasham wa Jimbo la Ulanga, Salim Hasham (kulia) katika ukaguzi wa shughuli za migodi katika Migodi ya Epanko Mahenge Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Mororogo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila alipofanya ziara katika Migodi ya Epanko inayochimba madini ya Spinel iliyopo Mahenge wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro ambapo amewataka wachimbaji wote wajitokeze kuhesabiwa ili serikali iweze kupanga mipango ya maendeleo katika Sekta ya Madini.

Prof. Msanjila amesema, kujitokeza kwao kutaiwezesha serikali kujipanga vizuri katika kuendeleza na kuboresha miundombinu katika maeneo ya uchimbaji wa madini.

"Akihesabiwa mchimbaji mmoja, serikali itajua anawatoto wangapi hivyo itasadia serikali kujua Sekta ya Madini inalea watu wangapi," amesema Prof. Msanjila.
Baadhi ya wafanyakazi wa migodi ya Epanko wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini ya vito aina ya Spinel wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila alipotembelea Migodi hiyo Mahenge wilaya ya Ulanga mkoani Mororogo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila wapili kutoka kushoto akizungumza jambo na Muwekezaji wa migodi ya Epanko ambaye pia ndiyo Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Hashm (kulia).
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Hasham baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya ukaguzi shughuli za madini wilayani humo.

Aidha, Prof. Msanjila amewasisitiza wachimbaji wa madini nchini kuchanja chanjo ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa UVICO-19 ambapo amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amejiridhisha kwamba chanjo ya ugonjwa huo ni salama na kuwataka wajitokeze kuchonja.

Pia, Prof. Msanjila amesisitiza suala la Usalama mahala pa kazi, ambapo amemtaka Afisa Migodi Mkazi wa Wilaya ya Ulanga Robert Erick kuhakikisha anafanya ukaguzi wa mara kwa mara katika migodi ya Epanko na kuwashauri wachimbaji kabla majanga hayajatokea ili kulinda afya zao.

Kufuatia hatua hiyo, Prof. Msanjila amesema, ili Wizara ya Madini ifanikiwe, lazima wachimbaji wa madini wafanikiwe ambapo amewashauri wachimbaji hao kujiunga kwenye vikundi na kushirikiana ili waliite Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuchoronga na kubainisha uelekeo wa mashapo ili kuepuka kuchimba kwa kubahatisha.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Wilaya ya Ulanga Robert Erick alipotembelea ofisi hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila Akizungumza jambo katika migodi ya Epanko wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini ya vito aina ya Spinel Mahenge wilaya ya Ulanga mkoa wa Mororogo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akizungumza jambo katika kikao chake na wafanyabiashara wakubwa wa madini ya vito waliopo Mahenge wilaya ya Ulanga mkoa wa Mororogo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa migodi ya Epanko wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini ya vito aina ya Spinel Mahenge wilaya ya Ulanga mkoa wa Mororogo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Migodi ya Epanko Mahenge wilaya ya Ulanga mkoa wa Mororogo.

Akijibu hoja ya Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Hasham, Prof. Msanjila amesema wilaya ya Ulanga inatarajia kupata uwekezaji mkubwa na wa kati katika uchimbaji wa madini ya _Graphite_ na kuahidi kushirikiana na Wizara ya Nishati ili isaidie kusogeza nishati ya umeme katika maeneo ya migodi ili kupunguza gharama za uzalishaji.

Vile vile, Prof. Msanjila amesema sehemu zote zenye milipuko ya madini wilayani humo lazima zirasimishwe haraka na kutolewa leseni katika maeneo hayo ili kuepuka migogoro isiyo kuwa ya lazima.

Pia, Prof. Msanjila amemtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro Emmanuel Shija kushirikiana na Afisa Migodi Mkazi wa wilaya ya Ulanga Robert Erick kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo wa madini ya Spinel juu ya kutunza kumbukumbu za biashara ya madini na kuwaunganisha na mabenki ili wapatiwe mikopo kwa lengo la kuimarisha shughuli za uchimbaji.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akiwa na baadhi ya viongozi wa Tume ya Madini pamoja na viongozi wa Migodi ya Epanko wakielekea kwenye ukaguzi wa shughuli za uchimbaji madini ya vito katika Migodi ya Epanko Mahenge wilaya ya Ulanga mkoa wa Mororogo.
Baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa madini ya vito wakifuatilia kikao cha Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila kilichofanyika Mahenge wilaya ya Ulanga mkoa wa Mororogo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akiwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samambe (Mbele), Mbunge wa jimbo la Ulanga Salim Hasham na baadhi ya wafanyakazi wa Migodi ya Epanko inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya vito aina ya Spinel iliopo Mahenge wilaya ya Ulanga mkoa wa Mororogo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akizungumza jambo katika eneo la migodi ya Epanko inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya vito aina ya Spinel iliyopo Mahenge wilaya ya Ulanga mkoa wa Mororogo.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Maudin Hasham amempongeza Prof. Msanjila baada ya kufanya ziara wilayani humo na kushuhudia mafanikio na changamoto zinazowakabili ambapo alimuomba Prof. Msanjila kusaidia upatikanaji wa nishati ya umeme na barabara bora kutoka Mahenge mpaka sehemu ya migodi.

Post a Comment

0 Comments