PSSSF washirikishwa faida lukuki za kupata chanjo ya UVIKO-19

Na Dennis Gondwe, DODOMA

CHANJO ya ugonjwa wa Uviko-19 ni muhimu kwa sababu inazuia kwa asilimia kubwa mtu asipate maambukizi na kuugua kufikia kiwango cha kuwekewa hewa ya OKSIJENI.
Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method alitoa elimu na kuhamasisha watumishi wa PSSSF kujacha

Kauli hiyo ilitolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method alipokuwa akitoa elimu na kuhamasisha watumishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) kwenye Bonanza la Wafanyazi Kujenga Afya lililofanyika katika uwanja wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dodoma.

Dkt, Method alisema kuwa mtu akipata chanjo ya ugonjwa wa Uviko-19 anakuwa salama. “Ukipata hii chanjo unakuwa salama. Chanjo inazuia wa asilimia kubwa usipate tena maambukizi. Na ikitokea umepata maambukizi, hautaenda kwenye ugonjwa utakaohitaji kwenda kuwekewa hewa ya ‘oxygen’” alisema Dkt. Method.

Mganga Mkuu huyo aliwataka watumishi wa mfuko huo kujitokeza kwa wingi na kuwashawishi wengine wajitokeze ili kupata chanjo. “Na sisi tutakuwepo hapa kuendelea kujibu maswali yote ambayo wanannchi wamekuwa nayo na sisi watumishi tumekuwa nayo ili muweze kufanya maamuzi sahihi ya kuchanja” alisema Dkt. Method.

Kwa upande wa Meneja wa Utawala wa PSSSF, Esther Mwamnyara alisema kuwa chanjo hiyo ni kwa ajili ya watu wote.

“Chanjo hiyo itaongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi, atatangulia kuchanja na kuzindua kwa niaba ya PSSSF. Kwa hiyo vijana wote mjitokeze, chanjo hii siyo kwa ajili ya wazee na vijana mjitokeze. Vijana ni taifa kesho” alisema Mwamnyara.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea na utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya chanjo ya Uviko-19 kwa kutembelea taasisi mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha na kutoa huduma ya chanjo kwa watakaohamasika ikiwa katika siku yake ya pili.

Post a Comment

0 Comments