Sabaya, wenzake kukata rufaa baada ya hukumu ya miaka 30 jela

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake watatu wanatarajia kukata rufaa baada ya kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Sabaya na wenzake wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akitoa hukumu hiyo leo Oktoba 15, 2021 Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo amesema ameridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka dhidi ya Sabaya na wenzake pasi na shaka.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hukumu hiyo, Wakili wa Sabaya na wenzake Mosses Mahuna amesema hawajaridhika na hukumu hiyo iliyotolewa kwa sababu ina upungufu mwingi.
Aidha, akisoma hukumu hiyo, Hakimu Omworo amesema, imethibitisha mshtakiwa wa kwanza (Sabaya) alikuwa na bastola ndani na nje kulikuwa na watu wawili wenye silaha hivyo, hakuna shaka duka la shahidi wa kwanza lilivamiwa na watu wenye silaha na lilikuwa chini ya watu wenye silaha.

Katika utetezi wake,Sabaya ameiomba mahakama imuonee huruma kwani sio yeye bali alikuwa anatekeleza maagizo ya Mamlaka yake ya uteuzi na ana mchumba walikuwa wafunge ndoa na mahari ameishalipa.

Baada ya washtakiwa kutiwa hatiani, Hakimu Amworo aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ndipo, Wakili wa Serikali, Felix Kwetukia akasema hawana kumbukumbu ya makosa ya zamani ya washtakiwa wote watatu na wameiomba Mahakama iwape adhabu ya miaka isiyopungua 30 jela na viboko.

Washtakiwa, Sabaya na wenzake walifikishwa mahakamani leo saa 3:05 asubuhi, kwa ajili ya hukumu ambapo Oktoba 1, 2021 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hukumu hiyo kwa maelezo ya kutokamilisha kuandika hukumu hiyo.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.  

Katika kesi hiyo, Sabaya alikuwa anatetewa na Wakili Moses Mahuna, Silvester Kahunduka na Wakili Fridolin Germelo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news