Shincheonji Church of Jesus Tanzania laendesha semina ya unabii wa kitabu cha Ufunuo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

OKTOBA 15 na 16, mwaka huu, Kanisa la Shincheonji Church of Jesus nchini Tanzania, liliandaa semina ya kitabu cha Ufunuo kwa ajili ya wachungaji na watumishi wa Mungu wa Tanzania, semina hiyo ilifanyika huko Kibada wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam katika Kanisa la Presbyterian na pia kwa njia ya mtandao wa zoom na youtube.
Takribani wachungaji 89 na waumini 201 walishiriki semina hiyo huko Kigamboni na kwa njia ya mtandao wa youtube pamoja na zoom, na kufanya jumla ya watu walioshiriki semina ya Oktoba 15, 2021 kuwa 290 na pia jumla ya watu walioudhuria Oktoba 16, 2021 walikuwa wachungaji 94 na waumini 194 na kufanya jumla wa watu 288.

Mwenyekiti wa Kanisa la Shincheonji Church of Jesus, Lee Man Hee ambaye ndiye alikuwa mhadhiri wa semina hiyo alisema “jukumu langu ni kufundisha na kushuhudia kitabu cha ufunuo ambacho nimeona na kusikia, ndio mimi mjumbe niliyetumwa kwa makanisa kushuhudia unabii wa kitabu hiki cha ufunuo.”

Mbali na semina hiyo, Shincheonji Church of Jesus, itaendeleza mafunzo ya semina ya kitabu cha ufunuo kwa muda wa siku 22, kuanzia Oktoba 18/10 mpaka tarehe 24/12 kwa njia ya youtube chaneli ya kanisa hilo.

Wachungaji walioudhuria walivutiwa sana na semina hiyo na kukubali kusaini hati ya makubaliano (memorandum of understanding), hati inayohusu makubaliano yasiyo ya kisheria kati ya makanisa yao na Kanisa la Shincheonji church of Jesus katika kueneza mafundisho hayo ya kitabu cha ufunuo.

“Makanisa machache yanaweza kufundisha vitabu vya unabii kama vile kitabu cha Daniel na kitabu cha Ufunuo japokuwa ndio vitabu muhimu sana kwa sababu vinaongelewa nyakati tulizo sasa ambazo ni nyakati za mwisho, kwa hiyo na mshukuru sana Mwenyekiti Lee Man Hee kwa kugundua huitaji wa watu kutaka kujua mafundisho ya kitabu cha Ufunuo, hii inamaanisha kuwa kuna kitu Mungu amempa ili aweze kuwapa watu wa Kigamboni na Dar es saam kwa ujumla,” alisema mchungaji Martin Antony Ndoyela kutoka Kanisa la EAGT Kisarawe.

Dkt.Nicolous Baibuka ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Pentecoste Kigamboni alisema, “kitabu cha Ufunuo ni muhimu sana ni neema kubwa sana kujua kitabu hiki, ndio maana nilivyosikia kuwa mtumishi wa Mungu atafundisha nilitaka kujua zaidi, Mwenyekiti Lee Man hee alisema hajawahi kwenda chuo, lakini alivyokuwa anafundisha niligundua vyote ni kama Biblia inavyosema, nimepata neema kubwa sana kusikia ufunuo, ningependa watu wengine wasikie ikiwemo na watoto wangu pia.”


Post a Comment

0 Comments