Simba SC,Azam FC, Biashara United zazidi kuibeba Tanzania michuano ya Kimataifa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Simba SC ambao ni mabingwa wa Tanzania, wameanza vyema michuano ya Afrika baada ya ushindi wa 2-0 ugenini.

Ushindi wao ni dhidi ya Jwaneng Galaxy baada ya kutupa karata yao katika dimba la Taifa jijini Gaborone nchini Botswana.
Mtanange huo wa Oktoba 17, 2021 mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, nahodha John Raphael Bocco ndiye aliyefunga mabao yote mawili dakika ya tatu na ya sita mara zote akimalizia mipira iliyookolewa baada ya kona.

Kwa matokeo hayo, Wekundu wa Msimbazi, watahitaji kuulinda ushindi wao kwenye mechi ya marudiano Oktoba 24, 2021 ili kwenda hatua ya makundi.

Wakati huo huo, Wanalambalamba, Azam FC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Pyramids katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika.

Mtanange huo ulipigwa katika dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Oktoba 16, 2021.
jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es

Azam FC kwa sare hiyo wamejipa kazi ya ziada kwenye mchezo wa marudiano Oktoba 23, mwaka huu katika dimba la Jeshi la Anga wa Juni 30 jijini Cairo nchini Misri.

Aidha, klabu hiyo inayonolewa na kocha Mzambia, George Lwandamina itahitaji ushindi au sare ya mabao ugenini ili kusonga mbele zaidi.

Awali Wanajeshi wa Mpakani,Biashara United kutoka mkoani Mara ilijiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya.

Ni baada ya kuonyesha kandanda safi katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa Oktoba 15, 2021 ambao ni wa kwanza Raundi ya Pili, mabao ya Biashara United inayofundishwa na kocha Mkenya, Patrick Odhiambo anayesaidiwa na mzawa, Marwa Chamberi yalifungwa na Deogratius Judika Mafie dakika ya 40 na Atupele Green Jackson dakika ya 61.

Mchezo wa marudiano utafanyika Oktoba 23,mwaka huu dimba la Martyrs of February mjini Benghazi nchini Libya.

Aidha,mshindi wa jumla atachuana na moja ya timu zitakazotolewa Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news