Spika Ndugai kufungua Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) kesho

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

SPIKA wa Bunge,Job Ndugai anatarajiwa kufungua rasmi Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) kesho jijini Dodoma ambapo mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi ya 150 yatashiriki katika wiki hiyo, lengo likiwa ni kuona mchango wa AZAKI kwa maendeleo ya Taifa.
Akiongea leo na waandishi wa habari jijini hapa, Nesia Mahenge ambaye ni Mkurugenzi Mkazi CBM Tanzania,amesema Wiki ya AZAKI itafanyika Oktoba 23 hadi 28, 2021 jijini Dodoma ambapo wiki hiyo itaambatana na maonesho mbalimbali ya kazi za AZAKI katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
"Kesho ni siku maalum na ni mwanzo wa siku ya AZAKI ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali zitakazoeleza mchango mkubwa watakaoenda kuufanya kwa amendeleo ya nchi yetu.

"Katika siku ya kwanza ya wiki ya AZAKI kuanzia saa moja asubuhi kutakuwa na matembezi kuanzia Shule ya Dodoma Sekondari hadi ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete ambapo ndio tutaenda kufanya ufunguzi wa wiki hiyo,"amesema Mahenge.

Pia amesema katika wiki hiyo kutakuwa na wageni mbalimbali kutoka mashirika ya ndani na nje ya nchi ambapo kwa upande wa viongozi wa kitaifa watakuwepo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka,Mstahiki Meya Devis Mwamfupe,Mkuu wa Wilaya, Jabiri Shekimweri,Msajili wa NGos na Mabalozi toka nchi mbalimbali ikiwemo Canada,Switzerland,Ubalozi wa Denmark kwa hapa nchini Tanzania.

"Pia kutakuwa na banda maalum kwa ajili ya utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 ambapo watu wenye uhitaji watachanja kwa hiari yao wenyewe na kuanzia tarehe 25 hadi 28 kutakuwa na majadiliano Royal Village tarehe 23 na 24,"amesema Mahenge.
Kwa upande wake Reynald Maeda Mkurugenzi Mtendaji UNA Tanzania akizungumzia AZAKI kwa ujumla amesema, AZAKI imeleta maendeleo katika sekta ya afya katika kuleta huduma ya afya karibu na wananchi masuala ya ujenzi wa vituo vya afya,kusomesha madaktari pamoja na vifaa,wamekuwa wakifuata miongozo mbalimbali ya Serikali kama wabia wanataka kufanya utafiti kupata picha kamili ili kuweza kuona mchango wa AZAKI kwa nchi ya Tanzania.

"Katika wiki hii Mashirika zaidi ya 150 yamejitokeza kushiriki katika wiki ya AZAKI ni ukweli usiopingika michango ya AZAKI imekuwa zaidi kama nchi pia Serikali imefanya juhudi katika kusaidia maendeleo ya nchi,kupitia wiki ya AZAKI ambayo ya kwanza yalianza 2018 kuangalia wanatoka wapi na kuangalia namna wanakuwa na michango ya nchi endelevu na kuhakikisha shughuli zao zinawafikia wananchi ili kuweka mikakati ya kujipima katika miaka ijayo na kuongeza nguvu," amesema Maeda.

Aidha, amesema matukio mengine ni utoaji wa tuzo kwa asasi za kiraia kutambua mchango wao katika maeneo wanayofanya kazi na mgeni rasmi atakuwa Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima na watafunga Wiki ya AZAKI siku ya Alhamisi tarehe 28.

Hata hivyo, maonesho hayo yataambatana na burudani mbalimbali kutoka wanamuziki wa kizazi kipya huku yakibebwa na kauli mbiu isemayo AZAKI kwa maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news