Ujumbe wa amani, upendo na mshikamano watawala Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaongoza waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na wananchi mbalimbali katika Maulidi ya kuadhimisha Kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) kitaifa yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman mjini Zanzibar.

Sherehe hizo za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambazo hufanyika kila mwaka Kitaifa hapa Zanzibar ni miongoni mwa kawaida na mila ya Waislamu wa Zanzibar.

Alhaj Dkt. Mwinyi ameungana na Waislamu na wananchi hao wakiwemo viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali pamoja na wananchi ambapo pia, Mama Mariam Mwinyi nae alihudhuria Maulid hiyo akiwa pamoja na viongozi wengine wanawake wa Kitaifa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj,Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitia ubani kuashiria kuaza kwa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika usiku wa Oktoba 18,2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitia ubani kuashiria kuaza kwa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika Oktoba 18, 2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na kushoto kwa Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora, Mhe.Haroun Ali Suleiman.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akitia ubani wakati wa hafla ya Maulidi ya kusherehekea Kuzaliwa kwa Mtume Muhammed (S.A.W) yaliyofanyika usiku wa Oktoba 18,2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na kulia kwake Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Mama Zuhura Kassim Ali na kushoto kwake Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Sharifa Omar Khalfan
Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakijumuika katika hafla ya Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika usiku Oktoba 18,2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman, Wilaya ya Mjini Unguja.
Ustadhi Hamdan Haji Hamdan kutoka Magogoni Wilaya ya Magharibi “B”Unguja, akisoma Quran Sura An Aam aya 44-48, kabla ya kuaza kwa Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja usiku wa Oktoba 18,2021.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akihudhuria Maulid ya kusherehekea Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (S.A.W) yaliyofanyika katika Uwanja wa Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja na kulia kwake ni Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Zuhura Kassim Ali na kushoto kwake ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Sharifa 0mar Khalfan. Wageni waalikwa Masheikh kutoka Nchini Misri walioko Zanzibar wakishiriki katika hafla ya sherehe za Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika uwanja wa Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja usiku Oktoba 18,2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar katika hafla ya kusherehekea Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika Uwanja wa Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja usiku Oktoba 18,2021 na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na kulia kwa Rais ni Mufti Mkuu wa Zanzaibar Sheikh. Saleh Omar Kabi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj. Othman Masoud Othman.
Ustadhi Khamis Ali Adam kutoka Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja akisoma Maulid ya Barzanji Mlango wa kwanza, katika hafla ya Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika usiku wa Oktoba 18,2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia hafla ya Maulid ya kusherehekea Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad(S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja usiku wa Oktoba 18,2021 kulia kwa Rais ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman na Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Saba Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Mhe.Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Ustadhi Nassor Seif Rashid kutoka Kibanda Hatari Wilaya ya Mjini Unguja akisoma Maulid ya Barzanji Mlango wa Nne wenye kisimamo na Sala ya Mtume Muhammad .S.A.W, wakati wa Maulid ya kusherehekea Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W yaliofanyika usiku wa Oktoba 18,2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman.

Wanafunzi kutoka Madrassatul Noor Ul Huda ya Fuoni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja wakisoma Qswida ya kumsalia Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika jana usiku katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja.
Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa katika kisimamo cha Qiyaam Wakimsalia Mtume Muhammad SAW, wakati wa Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika kisimamo cha Qiyaam na kumsalia Mtume Muhammad SAW, wakati wa hafla ya Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika jana usiku katika uwanja wa Maisara Suleiman na ( kulia kwake) Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Zuhura Kassim Ali na ( kushoto kwake) Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Sharifa Omar Khalfan na Mke wa Makamu wa Kwanza Mama Zainab Kombo Shaib. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika kisimamo cha Qiyaam na kumsalia Mtume Muhammad (S.A.W) katika Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.AW) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja usiku wa Oktoba 18, 2021, na kulia kwa Rais ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sheria,Katiba,Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Qasweeda ya Mwaka wa Kiislam Al Hijra 1443 na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Milade Nabii Association Zanzibar Bw. Sherali Champsi, wakati wa sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika jana usiku katika uwanja wa Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha zote na Ikulu).

Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Othman Ngwali alitumia fursa hiyo kuwakaribishwa wananchi wote pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika sherehe hizo za Maulid.

Katika Sherehe hizo, Waislamu walisisitizwa suala zima la amani, umoja na mshikamano miongoni mwao na kutakiwa kufuata nyayo za Mtume Muhammad (S.A.W) ili wapate kuongoka hapa duniani na kesho akhera.

Akisoma hotuba Sheikh Momammed Ali Mohammed kutoka Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, aliwataka Waislamu kuwa kitu kimoja huku akiwasisitiza umuhimu wa kusaidiana na kuhurumiana kwa lengo la kupata rehema za Allah.

Aidha, alieleza kuwa ni jukumu la Waislamu kusherehekea siku hii adhimu pamoja na kufuata mafunzo ya Mtume Muhammad (S.A.W) aliyokuja nayo.

Sherehe hizo za Maulid ambazo husherehekewa duniani kote, zilianza kufunguliwa na Qur-an tukufu iliyosomwa na Ustadhi Hamdan Haji Hamdan kutoka Magogoni na baadae kuendelea kusomwa Milango ya Barzanj pamoja na Qaswida kutoka madrasa mbalimbali za Zanzibar yakiwemo Maulid ya Hom kutoka Jumuiya ya Maulid ya Hom Mtendeni, Mkoa wa Mjini Magharibi ambayo nayo yalikuwa kivutio kikubwa katika sherehe hizo adhimu.

Akisoma historia fupi ya Maulid hapa Zanzibar Mshauri Mkuu wa Kamati ya Maandalizi Sheikh Sherali Chapsi alisema kuwa shughuli hizo za Maulid hapa Zanzibar zimeanzishwa mapema mnamo mwaka 1926 kwa ushirikiano wa Waislamu wote wanaoishi hapa Zanzibar.

Aliongeza kuwa, Jumuiya ya Milade Nabii hapa Zanzibar iliundwa kwa dhamira ya kuwaunganisha Waislamu na kusimamia sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), ambapo mwaka huu 2021 inatimiza miaka 96 ya usimamizi wa shughuli za Maulid, wakati huo huo Sheikh Sherali Chapsi akitumia fursa hiyo kumkabidhi Alhaj Dkt. Mwinyi Qasweeda ya mwaka 1443 Alhijra.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news