Mashindano ya Dkt.Kimea Cup yafikia tamati, Waziri atoa rai kwa mashabiki

NA PROJESTUS BUNAMUNGU

WAZIRI wa Utamaduni, Sana na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ameonya tabia ya mashabiki wa timu kubeza timu zao pindi zinaposhindwa kufikia malengo au hatua iliyotamaniwa na mashabiki husika akisema kitendo hicho siyo cha kizalendo na kinawavunja moyo wachezaji.
Picha mbalimbali za wachezaji wa timu za Kwamndolwa na Mgombezi wakati wa mchezo wa fainali ya mashindano ya Dkt.Kimea Cup katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Korogwe TCC, Novemba 21, 2022.

Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, katika kilele cha mashindano ya mpira wa miguu wa jimbo la Korogwe yaliyopewa jina la Dkt. Kimea Cup

Waziri Bashungwa amesema Watanzania hawana budi kutambua kuwa michezo mingi umalizika kwa matokeo ya aina tatu, ambayo ni kufunga, kufungwa na kutoa sare, hivyo mashabiki hawana budi kuwa tayari kuyapokea matokeo yote matatu.
Waziri wa Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akifuatilia mchezo baina ya timu za mpira wa miguu kutoka kata za Kwamndolwa na Mgombezi katika mchezo wa fainali ya mashindano ya Dkt. Kimea Cup katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Korogwe TCC, Novemba 21, 2022. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Emmanuel Charles na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mji Dkt. Alfred Kimea

Waziri wa Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akisalimiana na wa timu za kata ya Kwamndolwa na kata ya Mgombezi wakati wa kilele cha mashindano ya Dkt. Kimea Cup katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Korogwe TCC, Novemba 21, 2022.

“Nyinyi nyote mnaoshindana leo ni wazuri ndiyo maana mmefikia fainali, hivyo nyote ni wangu lakini lazima mjue kwamba kwenye mchezo wa mpira wa miguu kuna kushinda, kushindwa na kupata sare, yote ni matokeo na yote lazima watanzania tuwe tayari kuyapokea” alisema Waziri Bashungwa wakati akizungumza kabla ya mchezo baina ya timu mbili zilizoingia fainali katika mashindano hayo.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Korogwe Mji Dkt. Alfred Kimea amesema mashindano hayo yameinua vipaji vya vijana wengi katika jimbo la Korogwe mji, ambavyo atahakikisha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali wanaendeleza vipaji hivyo vya soka kwa manufaa ya vijana na jamii nzima ya Korogwe na Tanga kwa ujumla.
Waziri wa Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na wachezaji wa timu za kata ya Kwamndolwa na kata ya Mgombezi (hawapo pichani) wakati wa kilele cha mashindano ya Dkt. Kimea Cup katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Korogwe TCC, Novemba 21, 2022, kulia kwake ni Mbunge wa jimbo la Korogwe Mji Dkt. Alfred Kimea.

Mashindano ya Dkt. Kimea Cup yalishirikisha timu 12 kutoka kwenye kata 11 za Jimbo la Korogwe mji na kuziwezesha timu ya kata ya Kwamndolwa na kata ya Mgombezi kuingia katika fainali ya mashindano hayo, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Korogwe (Korogwe TCC) Novemba 21, 2021.
Waziri wa Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na Mbunge wa jimbo la Korogwe Mji Dkt. Alfred Kimea katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu za kata ya Kwamndolwa na kata ya Mgombezi mapema kabla ya mchezo wakati wa kilele cha mashindano ya Dkt. Kimea Cup katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Korogwe TCC, Novemba 21, 2022.

Post a Comment

0 Comments