Serikali, Swiss TPH waja na mbinu mpya kutokomeza Malaria nchini

NA HADIJA BAGASHA

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria kwa kushirikiana na SWISS TPH mradi wa TEMT unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi umewajengea uwezo viongozi zaidi ya 512 wa Serikali za kata na Mitaa wakiwamo Wenyeviti na Watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa lengo la kuhakikisha ugonjwa wa malaria unatokomezwa nchini.
Dkt.Denis Kailembo ambaye ni Mratibu wa Mradi wa TEMT kutoka Shirika la SWISS TPH akizungumza na waamdishi wa habari jijini Tanga juu ya namna walivyojipamga kuutokomeza ugonjwa wa malaria.
Awali akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa awamu mbili kwa nadharia na vitendo jijini hapa, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Abdurhaman Shiloo aliwataka viongozi hao waliopata mafunzo hayo kwenda kuyatumia ipasavyo ili kuisaidia Jamii kutokomeza malaria.

Amesema, endapo kila mmoja atawajibika ipasavyo katika jamii ugonjwa wa Malaria mkoani hapa utakuwa historia.

"Kila mmoja wetu endapo atawajibika ipasavyo basi malaria nchini kwetu itakuwa historia, lakini pia mbu hawa ambao tumejifunza hawaenezi malaria peke yake wanaeneza magonjwa mengi, hivyo kama tutaenda kuua mazalia ya mbu tutakuwa tumeokoka na magonjwa mengi sana yanayotokana na mbu,"amesisitiza Shiloo.
Kwa upande wake Dkt.Denis Kailembo ambaye ni Mratibu wa Mradi wa TEMT kutoka Shirika la SWISS TPH alisema, mradi huo unatekelezwa kwenye halmashauri 15 nchini.

"Kwa Mkoa wa Tanga mradi huu unatekelezwa kwenye halmashauri tatu ambazo ni Tanga Jiji,Handeni Vijijini na Lushoto, tayari tumefanya kwa wakufunzi ngazi ya Mkoa na Halmashauri na uhamasishaji kwa ngazi hizo ulishafanyika tayari na sasa tupo ngazi ya kata na mitaa,"amesema Dkt.Kailembo.
Dkt.Kailembo alisema mafunzo hayo kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga yameshirikisha washiriki kutoka kata zote 27, Mitaa 181 ambapo Washiriki 512 wameweza kupatiwa mafunzo hayo lengo likiwa kuhakikisha hadi ifikapo 2030 ugonjwa wa malaria uwe umetokomezwa kabisa.

"Tunategemea mafanikio makubwa kutokana na mafunzo haya na endapo utekelezaji utafanyika kikamilifu basi Mpango wa Taifa wa kutokomeza Malaria nchini ifikapo 2030 utatimia mapema,"alisisitiza Dkt.Denis.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news