Balozi Meja Jenerali mstaafu Issa Suleiman Nassor atembelea vyanzo vya maji vya ZAWA Kusini Unguja

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Balozi Meja Jenerali mstaafu Issa Suleiman Nassor leo ameendelea na ziara yake siku ya pili kwa kutembelea maeneo ya vyanzo vya maji vya ZAWA Mkoa wa Kusini Unguja.
Balozi Meja Jenerali Mstaafu Issa Suleiman Nassor, ametembelea chanzo cha maji safi na salama ya Machomwe Kizimkazi, kinachozalisha maji na kusambaza katika kijiji hicho.

Aidha, ametembelea visima vya maji vya Makunduchi, Jambiani Mfumbwi, Kijuuni na Kivulini.

Pia, ametembelea kisima cha maji cha Bwejuu – Michamvi na Ukongoroni.
Akifanya majumuisho baada ya ziara hiyo, Balozi Meja Jenerali Mstaafu Issa Suleiman Nassor amesema,watendaji wa ZAWA wanatakiwa kuboresha huduma ya maji safi na salama pamoja na kushirikiana vyema na taasisi nyingine ili kutatua baadhi ya changamoto zilizopo katika maeneo hayo.

Post a Comment

0 Comments