Bilionea Mo Dewji aweka mezani Bilioni 2/- ujenzi uwanja wa Simba SC

NA GODFREY NNKO

BILIONEA Mohammed Dewji ambaye ni mwekezaji katika Klabu ya Simba ameweka mezani Shilingi Bilioni 2 kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa dimba la klabu hiyo.
Ndani ya Simba SC, Mo Dewji ana asilimia 49 ya hisa ambazo anapewa mwekezaji katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo.

Katika ukurasa wake wa Mtandao wa kijamii ameandika, "Nimepokea maoni mengi ya WanaSimba wenzangu wakishauri tujenge uwanja wetu na wako tayari kuchangia ili tufanikishe ujenzi huo. Naomba kuweka wazi kwamba nimepokea maoni hayo kwa mikono miwili.
"Naomba Bodi ya Simba kukaa na kuja na utaratibu wa haraka ili jambo hili lianze utekelezaji. Kwa kuanza naahidi kuchangia Tsh. 2 bilioni. Nawaomba wanasimba tuchangie sote,"amesema Mo Dewji.

Klabu hiyo ina uwanja wao maarufu kama Mo Simba Arena uliopo Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news