Bilioni 1.7/- zajenga vyumba vya madarasa 87 wilayani Nzega

NA NTEGHENJWA HOSSEAH,OR-TAMISEMI

HALMASHAURI ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora imefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa ya Sekondari 87 ambavyo vimegharimu Shilingi Bilioni 1.74, fedha kutoka kwenye Mradi wa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya Uviko-19.
Fedha walizozipata mwezi Oktoba,2021 zimefanikisha ujenzi wa vyumba 87 ambavyo vimekamilika na vitawezesha asilimia 56 ya wanafunzi waliofaulu darasa la saba kuanza kidato cha kwanza kwa awamu moja.

Akiwa ziarani wilayani humo, Mhe. Ummy Mwalimu amekagua madarasa matatu yaliyojengwa kwenye shule ya Sekondari Kampala kwa niana ya madarasa yote 87 yaliyojengwa katika halmashauri hiyo.
Mhe. Ummy ameridhwa na ubora wa vyumba hivyo vya madarasa na amewapongeza kwa usimamizi makini uliofanikisha ukamilishaji wa vyumba vya madarasa hayo. 
Kwa upande wa Vituo shikizi Halmashauri ya Wilaya ya Nzega walipata shilingi Milioni 580 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 29 kwenye vituo shikizi.

Post a Comment

0 Comments