Makachero wanasa wauzaji madini feki

NA LUCAS RAPHAEL

MWANAMKE mmoja mkazi wa mkoani wa Arusha amekamatwa na Jeshi la Polisi katika stendi ya mabasi wilayani Sikonge mkoani Tabora kwa tuhuma za kukutwa na madini feki aina ya dhahabu waliyokuwa wakiwauzia wananchi wa kishrikiana na dereva wake.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, ACP Richard Abwao amesema, walimkamata Mariam Said, mkazi wa Arusha akiwa na dereva wake, David George wakiwa na madini hayo waliyoyatumia kumtapeli mkazi wa Kijiji cha Usunga wilayani humo aitwaye Edward.

Alibainisha kuwa, watuhumiwa walikamatwa baada ya kumtapeli mkazi huyo kiasi cha sh.340,000 ambapo pia baada ya kukaguliwa walikutwa na kadi tano za benki tofauti tofauti ambazo ni kadi za NMB 3, Posta 1na CRDB 1.

Vitu vinginevyo walivyokutwa navyo ni simu 4 aina ya iphone 6s plus, Tecno Spark 5 Air, Infinix hot 10 na Samsung zinazodhaniwa kuwa za wizi.
Kamanda Abwao amebainisha kuwa, madini hayo yamekamatwa kutokana na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuzuia, kutanzua na kupambana na uhalifu.

Aidha, ameongeza kuwa katika kukabiliana na matukio ya uhalifu, mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha, ujambazi na uvunjaji mkoani humo, jeshi hilo limeendelea kufanya operesheni mbalimbali katika wilaya zote.

Alitaja mafanikio ya operesheni hiyo kwa mwezi huu kuwa ni kukamatwa watu wawili, Khamis Baruti na Mohamed Shaban wakazi wa Izimbili wilayani Uyui kwa kukutwa na silaha aina ya gobore isiyo na namba za usajili iliyokuwa ikitumika kwenye uwindaji haramu.
Aidha, walikamata silaha mbili aina gobore zilizosalimishwa na watu wasiojulikana katika kata za Kipanga na Mole ( Usanganya) wilayani Sikonge na silaha nyingine ilisalimishwa na mkazi wa Mibono John Matuzya katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kiloleni akidai anatii sheria bila shuruti.

Kamanda alitoa wito kwa wananchi wanazomiliki silaha kinyume na utaratibu kuendelea kuzisalimisha ndani ya kipindi hiki cha msamaha wa Waziri wa Ulinzi vinginevyo watakamatwa, aliitaka jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za vitendo vya uhalifu na wahalifu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news