TANESCO:Tunaendelea na mkakati wa matumizi ya vyanzo mseto vya uzalishaji umeme

NA MWANDISHI MAALUM

SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) limesema kuwa, wanaendelea na mikakati kabambe ya kutumia vyanzo mseto kwa ajili ya uzalishaji umeme nchini.

Hayo yamesemwa Desemba 13, 2021 na wataalam kutoka shirika hilo akiwemo Meneja Uhusiano, Johary Kachwamba na Afisa Mkuu Huduma kwa Wateja, Martin Mwambene wakati wakipokea maoni na kujibu maswali katika kipindi cha Kumepambazuka cha Redio One Stereo.
"Tunaendelea na mkakati wa matumizi ya vyanzo mseto vya uzalishaji umeme ambapo mpaka sasa gesi inachangia asilimia 56, maji asilimia 36, fungamo taka asilimia moja na mafuta asilimia saba kwenye maeneo ambayo bado hayajafikiwa na Gridi ya Taifa,"wamebainisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news