Tanzia ya Askofu wa Calvary Assemblies of God,Zephania Ryoba

NA BENJAMIN KENDINGO GWAMISONIFIIJO

KATIBU Mkuu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God,(CAG), Bishop Zephania Ryoba ametangulia mbele ya haki Jumanne,Desemba 14,2021.
Taarifa kutoka katika kanisa hilo imesema "Huu ni msiba mkubwa kwetu kwani Baba yetu mpendwa amelala".

Bishop Ryoba aliliongoza kanisa hilo lenye makao makuu yake mjini Morogoro, kama Katibu Mkuu.Askofu Mkuu wa kanisa hilo ni Danstan Maboya.

Bishop Ryoba sambamba na utumishi huo, kwa miaka mingi ya uhai wake alikuwa Mhadhiri wa Chuo cha Kilimo SUA.

"Alianzia kazi academis(Mhadhiri),kisha akawa administrator, kisha akawa Dean of Students na mpaka anastaafu alikuwa Katibu wa Baraza la SUA," chanzo cha habari cha kanisa hilo kimefafanua.

Mzee Ryoba ambaye waumini wa kanisa hilo walipenda kumuita Baba, baada ya kustaafu kwake utumishi wa umma alijikita zaidi kumtumikia Mungu kama Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo kwenye makao makuu yake yaliyopo eneo la Kikundi,Barabara ya SUA,Mjini Morogoro.

Kwa miaka mingi mpaka sasa Calvary Assemblies of God ni moja ya makanisa nchini ambayo waumini wake wanaongoza kwa kumiliki digrii nyingi,wengi wao wakiwa ni Wanataaluma kutoka vyuo vikuu vya mjini humo hususani SUA,Mzumbe n.k, lakini wakiwa wanyenyekevu kupindukia.

R.I.P Mzee Ryoba siku zote hakupenda kujikweza, wala kuitwa kiongozi wa kanisa zaidi ya kuitwa Mchungaji tu.

Marehemu Bishop Ryoba ameacha watoto wanne kwenye ndoa yake na mkewe Dk.Ruth Ryoba ambaye ni Mhadhiri Mwanandamizi SUA.

Waumini wa kanisa hilo wakimuelezea Dk. Ruth wanasema ni mtii sana mnyenyekevu kwa mumewe na kanisa kwa ujumla na kwamba amekuwa nguzo kuu katika utumishi akiwa mama bora wa kupigiwa mfano na wanawake wengi.

Sambamba na utumishi wa umma, Dk. Ruth Ryoba ni Mkurugenzi wa mtandao wa wanawake wa kanisa hilo lijulikanao kama JEWAWI, yaani Jeshi la Wanawake Wapelekao Injili Tanzania.

Jewawi limekuwa msaada mkubwa kwa wanawake wengi ambao kwa sasa wengine ni ma Profesa,Madaktari wa wa Falsafa walio wengi, wakurugenzi,wabunge wakiwa wametapakaa kotekote nchini.

Taarifa za maziko ya marehemu Bishop Ryoba zitawajia baadaye.

Bwana alitoa na tena ametwaa jina lake lihimidiwe.

Imeandaliwa na Mfuasi wa Yesu Benjamin Kendingo Gwamisonifiijo, ambaye aliwahi kusali katika kanisa hilo miaka ya nyuma akiwa masomoni Mjini Morogoro

Post a Comment

0 Comments