Makamu wa Kwanza wa Rais aungana na waumini kuusalia mwili wa marehemu Ali Sultan Issa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman ameungana na waumini wa dini ya kiislam katika sala ya kuusalia mwili wa mwanasiasa mkongwe Zanzibar, marehemu Ali Sultan Issa.

Issa wakati wa uhai wake aliwahi kuwa Waziri pamoja na kushika nyadhifa nyingine kadhaa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Marehemu amefariki dunia jana na kuswalia leo huko Masjid Rahman, Kijichi maskani Wilaya ya Magharib 'A' Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jijini Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments