Mkuranga wakamilisha ujenzi wa madarasa 146

NA MWANDISHI MAALUM

UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani umekamilisha ujenzi wa madarasa 146 waliyopatiwa fedha na Serikali kupitia mradi wa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Akizungumza katika makabidhiano ya madarasa hayo yaliyofanyika katika Kituo Shikizi cha Lugwadu Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mhe. Khadija Nassir Alli ameitaka jamii ya Mkuranga kutunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kuendelea kunufaisha jamii ya Mkuranga.

Pia amewataka wazazi na walezi wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanahamasisha watoto wao kwenda shuleni ili kupata elimu bora itakayowakomboa katika maisha yao.

“Madarasa haya yamejengwa kwa ajili ya watoto wetu sasa wasipokuja shule miundombinu hii haitakua na maana hivyo kila mzazi au mlezi ahakikishe mtoto wake anakwenda shule awe ni wa madarasa ya awali, darasa la kwanza au sekondari,"amesema Khadija.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mwantumu Mgonja amesema walipokea shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Sekondari 116 sambamba na yake ya vituo shikizi 30 ambayo mpaka kufikia leo hii ujenzi umekamilika kwa asilimia 96.

Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha hizo zilizomaliza kabisa changamoto ya vyumba vya madarasa.
"Kwa mwaka 2021 wanafunzi waliomaliza kidato cha nne ni 2,000 na waliochaguliw kujiunga na kidato cha kwanza ni 7,122 hivyo tulikuwa na ongezeko la wanafunzi takribani 5,000.

"Tusingepata fedha za ujenzi wa vyumba hivi sijui hawa watoto wote tungewapeleka wapi lakini kwa sasa tuna uhakika kuwa wanafunzi wote wataanza kidato cha kwanza kwa awamu moja,"amesema Mgonja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news