RAIS WETU SAMIA, SISI TWAKUFURAHIA

LEO tunafurahia, bethidei yako mama,

Mungu amekujalia, mwaka mpya huu mama,

Na kiti umekalia, twakufurahia mama,

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.
Sisi twakufurahia, siku yako hii mama,

Sababu watufanyia, mengi ni mazuri mama,

Mbele tukiangalia, mambo yatakuwa mema,

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.


>Kile unachovutia, hadi hivi leo mama,

Ni yale watuambia, kwa hotuba zako mama,

Twaona yanatimia, tunakushukuru mama,

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.


>Kitu umetufanyia, ni kikubwa sana mama,

Ni wengi kimetujia, twafurahi sana mama,

Hata tunafikiria, alikuwa wapi mama?

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.


>Mwaka unapoishia, mara nyingi huwa noma,

Watoto wanazidia, kutaka elimu njema,

Mwisho kinachobakia, kukosekana huduma,

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.


>Januari kuanzia, watoto wanze kusoma,

Nyuma tukukikumbukia, kwa mafungu walisoma,

Madarasa kutumia, idadi yao likwama,

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.


>Wengine ilifikia, Machi waanza kusoma,

Ni kweli kusingizia, ufaulu kuwa nyuma,

Lakini sasa sikia, amesimamia mama,

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.


>Mwaka huu sikizia, watoto wote kusoma,

Madarasa meingia, yote yakiwa ni mema,

Uongozi mechangia, sote kuweza simama,

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.


>Hongera Mama Samia, kusimamia u vema,

Pesa tulijipatia, sasa watoto wasoma,

Jinsi tulivyotumia, matokeo yake mema,

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.


>Hapo ulipofikia, mpango wa Mungu mama,

Wala hujajitakia, taratibu zasimama,

Heri tunakutakia, uzidi tumika mama,

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.


>Heri tunakutakia, na maisha mema mama,

Mungu alokupangia, uyakamilishe mama,

Miaka ya kuzidia, pia ujaliwe mama,

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.


>Wito tumeusikia, ulioutoa mama,

Uchumi kuuchangia, tuzifanye kazi vema,

Mama tumekusikia, tunakushukuru mama,

Rais wetu Samia, hapi bethidei kwako.




Na Lwaga Mwambande (KiMPAB)

27/1/2022

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news