Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Januari 3, 2022

NA GODFREY NNKO

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imewatakia Watanzania wote na wadau mbalimbali wa maendeleo hapa nchini heri ya Mwaka Mpya 2022 huku ikisisitiza kuwa,itaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha ili kuwezesha ustawi wa maendeleo endelevu nchini.
Mbali na hayo leo Januari 3, 2022 BoT imetoa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha mbalimbali za kigeni.

Mosi kwa mujibu wa BoT, leo dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2,286.18 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.04.

Pili kwa upande wa Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3081.997 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3113.74.

Tatu kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2589.55 na kuuzwa kwa shilingi 2615.68. 

Kwa upande wa Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.97 huku ikiuzwa kwa shilingi 363.46 huku Yen ya Japan ikinunuliwa kwa shilingi 19.86 na kuuzwa kwa shilingi 20.051.

Wakati huo huo, kwa mujibu wa BoT, Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 143.37 na kuuzwa kwa shilingi 144.72 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.223 na kuuzwa kwa shilingi 20.39.

Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.

Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.205. Kwa taarifa zaidi kuhusu viwango vingine, endelea hapa chini;

Post a Comment

0 Comments