Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Januari 26, 2022

NA GODFREY NNKO

FRANKA ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa shilingi 2286.57 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.44.
Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2577.198 na kuuzwa kwa shilingi 2603.43 huku Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3076.81 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3108.51.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Januari 26, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kwa mujibu wa BoT, Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 361.27 huku ikiuzwa kwa shilingi 364.84 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 20.06 na kuuzwa kwa shilingi 20.26.
Wakati huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.624 na kuuzwa kwa shilingi 0.654.

Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 149.28 na kuuzwa kwa shilingi 150.66 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.155 na kuuzwa kwa shilingi 20.32.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news