Ziwani wafanya hujuma kwa kutoboa bomba la maji safi na salama

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Maji Pemba imeelezea kusikitishwa na kitendo cha wananchi wa Ziwani kutoboa bomba la nchi nne kwa kujihusisha na umwagiliaji mboga mboga uliokithiri

Kadhia hiyo imepelekea malalamiko makubwa ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Shehia ya Ziwani ikijumuisha vijiji vya Kiwapwa, Mchangakwale, Jitenge, Mavungwa, na Barawa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, tayari imechukuwa hatua ya kurekebisha kadhia hiyo.

"Huduma imerejea vizuri kwa jamii na tumeripoti katika vyombo vya sheria ili yeyote atakayebainika na hatia, sheria ichukuwe mkondo wake,"imeeleza mamlaka hiyo.

Post a Comment

0 Comments