Rais Dkt.Mwinyi alivyozindua Kongamano la Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Wazazi Tanzania

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka wanaCCM kujibu hoja kwa vitendo badala ya maneno, kwani wana dhima kubwa ya kuendeleza amani iliyopo nchini.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Machi 26,2022 huko katika ukumbi wa CCM Amani Mkoa, katika uzinduzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Wazazi Tanzania, ambalo kitaifa mwaka huu linafanyika hapa Zanzibar.
Katika maelezo yake, Rais Dkt.Mwinyi alieleza kwamba hivi karibuni wametokea baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitoa maneno maneno juu yake na Serikali anayoiongoza na kusema kwamba ni vyema watu hao wakajibiwa kwa vitendo badala ya maneno.
Rais Dkt.Mwinyi ambaye pia ni Mjumbe wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, aliwataka wanaCCM kuwa na subira huku Serikali anayoiongoza ikitekeleza majukumu yake ipasavyo sambamba na chama chao kikiendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 kwa vitendo.

Post a Comment

0 Comments