Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Aprili 11,2022

NA GODFREY NNKO

SHILINGI ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.8 na kuuzwa kwa shilingi 20.001 huku Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.22 na kuuzwa kwa shilingi 2.29.

Yen ya Japan (JPY) inanunuliwa kwa shilingi 18.4 na kuuzwa kwa shilingi 18.5 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 155.3 na kuuzwa kwa shilingi 156.9.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Aprili 11, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.

Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2287.2 na kuuzwa kwa shilingi 2310.1 huku Paundi ya Uingereza (GBP) ikinunuliwa kwa shilingi 2979.3 na kuuzwa kwa shilingi 3010.02.

Aidha,Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2484.1 na kuuzwa kwa shilingi 2509.9 huku Yuan ya China (CNY) ikinunuliwa kwa shilingi 359.4 na kuuzwa kwa shilingi 363.001.
Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.8 na kuuzwa kwa shilingi 628.8 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) inanunuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.1.

Kwa upande wa Dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1706.02 na kuuzwa kwa shilingi 1723.5 huku Pula ya Botswana (BWP) inanunuliwa kwa shilingi 197.6 na kuuzwa kwa shilingi 200.05.
Kwa mujibu wa Benki Kuu, dola ya Canada (CAD) inanunuliwa kwa shilingi 1816.97 na kuuzwa kwa shilingi 1834.5 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.06 na kuuzwa kwa shilingi 50.51.

Post a Comment

0 Comments