Mbowe,wenzake CHADEMA wahukumiwa kulipa milioni 350/-

KISUTU,Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemuhukumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na wenzake kulipa faini ya sh.milioni 350 ama kwenda jela miezi mitano baada ya kutiwa hatiani kwenye makosa 12 ikiwemo la kufanya maandamano.

Hukumu hiyo iliyochukua takribani saa nne, kuanzia saa saba mchana hadi saa 11 jioni, imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi 23 baina ya utetezi na Serikali.

Katika hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema amewatia hatiani washitakiwa katika mashitaka 12 kati ya 13.

Kosa ambalo hawajatiwa nalo hatiani ni kosa la kwanza ambalo ni kufanya mkusanyiko usio halali.
BREAKING: Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA Wahukumiwa Kulipa Faini ya Milioni 350 Au Kwenda Jela
“Mashitaka waliyotiwa hatiani ni mabaya katika jamii ukizingatia wao ni viongozi na walitakiwa kuwa mstari wa mbele katika utii wa sheria, hivyo Mahakama inaona kuwa wanastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine watakaofanya makosa kama haya.

“Natoa adhabu kali kwa kuzingatia hoja ya kuwa washitakiwa ni wakosaji wa kwanza na wanatakiwa kupewa huruma na ukizingatia wengine walishakaa mahabusu, hivyo kukaa kwao ndani ni adhabu tosha kwa mantiki hiyo nawaepusha na adhabu ya vifungo kwa washitakiwa wote,”alieleza Hakimu huyo mbele ya Mahakama.
Katika adhabu hiyo, Mbowe amehukumiwa kulipa sh.milioni 70, Halima Mdee sh.milioni 40, Dkt.Mashinji kulipa sh.milioni 30, John Heche sh.milioni 40,Mchungaji Msigwa sh.milioni 40, Ester Bulaya sh.milioni 40, John Mnyika sh.milioni 30, Salum Mwalimu sh.milioni 30 na Ester Matiko sh.milioni 30.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news