Magazeti leo Januari 28,2026

TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tarehe 27 Januari, 2026, imekutana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu (CDF),Venance Mabeyo.
Mkutano huo wa tume na Mabeyo umefanyika katika Ukumbi wa Tanganyika uliopo katika ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini, Dar es Salaam.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.

Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo ikiwa na lengo la kupata kiini cha chanzo cha matukio hayo na kuyawasilisha kwa ajili ya hatua zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here